Msanii FEROUZ amekamatwa na bangi

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Vijana ni nguvu kazi ya taifa, lakini vijana hao hao wanaweza kuwa chanzo cha taifa kutoendelea na kubomoka. Ubomoaji wa taifa
huwa kwa namna nyingi ikiwemo uvivu,ufisadi, na kadha wa kadha.Lakini hapa,tuangalie hili la madawa ya kulevya na bangi.

Kila kukicha kuna wasanii wa maigizo na filamu ambao tunasikia wamekamatwa na madawa ya kulevya, "unga" katika jitihada za
'kusaka maisha', wenyewe wanasema kuna ajali kazini. Wasanii hao ambao wengi ni vijana, na pale wanapoonekana kwenye runinga huwa hamasa kwa wadogo zao na jamii kwa ujumla,wakipenda kuwa kama wao.

Na mchana huu, maeneo ya Sinza, kuna taarifa ya mwanamuziki aliyetamba kwenye muziki wa bongo fleva, Ferouz, sanasana kwa
wimbo wake wa Starehe, ambao ulikuwa ukionyesha madhara ya UKIMWI na virusi vya UKIMWI.

Ferouz anadaiwa kukutwa na bangi,na picha ambazo Gospel Kitaa imezipata eneo la tukio, zinamuonyesha akisindikizwa na maafande kunako mbele ya vyombo husika.

Vijana wa Tanzania tuna shida gani? Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu tunazo, sasa nini shida zaidi? Ipo haja ya Operesheni ambazo Askofu Sylvester Gamanywa ameitisha za Takasika iliyomalizika hivi karibuni, na kisha kupokelewa na Operesheni Milikisha,
kuwahusisha pia wasanii wa aina zote, maana wanaonekana kukumbwa na janga hili kwa sana, vinginevyo, vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa watakuwa wakijaa jela za ndani na nje,wakiacha wageni kuja kutawala.

Askari wakiwa wamemzingira.

CHANZO: Gospel Kitaa
 
Vijana wanatamaa ya kupata utajiri haraka haraka. Mbona hujaweka picha? Na imani hii kesi itapotezewa tu maana hata twenty percent alilipotiwa na vyombo vya habari kukamatwa na bangi akiwa njiani kwenda pwani kesi yake iliyeyuka hadi leo sijasikia tena. HII NDIO TZ BWANA.
 
Wauza unga hawakamatwi kila siku wanakamatwa wauza bangi
 
Kwani msanii kuvuta bhanghe ni kosa!!?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Najua kwa walala hoi mtaandika habari huku migongo ikiwavuja jasho lkn habar za muhimu hamna lolote.
 
Bangi sio mbaya,nashangaa kuna wajinga wanaiita dawa za kulevya.
 

hamna kesi hapo wewe hao mwera unawapa buku 2 wanapotea alafu na nyie mwera aka police mnatakiwa mtulinde na sio kutuwinda..chaukucha dawa!
 
Hiyo bange aliyokutwa nayo jamaa, ni misokoto ya kuvuta yeye tuu au ni mzigo wa kwenda kuusukuma!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…