Msanii G LUCK

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
Vipi hii historia unaikumbuka.

GCB KUNDI LA MUZIKI TOKA MKOANI SONGEA.
________________________

GCB ni moja Kati ya makundi ya mwanzo kabisa Nchini Tanzania kufanya Muziki kutokea mkoani "Songea"

GCB ilikua ni kifupisho Cha majina ya wasanii waliounda kundi hilo ..

๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ G-G luck
๐Ÿ‘‰๐ŸฟC-Cammy boy
๐Ÿ‘‰๐ŸฟB -Bad H

Huko mkoani Songea kundi Hili walifanikiwa kufanya kazi na Producer "jof master"

Kundi hili Enzi Hizo liliundwa na vichwa vitatu (3) ambavyo ni:

๐Ÿ‘‰๐ŸฟG luck,
๐Ÿ‘‰๐ŸฟCammy
๐Ÿ‘‰๐ŸฟBad H

Kundi Hili limekwisha fanya kazi nyingi sana

Lakini pia walifanya kazi na wasanii wengine ( collabo) kama vile

๐Ÿ‘‰๐ŸฟNEY WA MITEGO
๐Ÿ‘‰๐ŸฟENDRU G
๐Ÿ‘‰๐ŸฟPASHA
๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ PNC

Na wengine wengi..

Wasanii wengi wa zamani Enzi Hizo walilazimika kusafiri kutoka mikoani hadi jijini Dar es salaam ili waweze kurekondi Kazi zao.

Lakini wao walifanya project nyingi na zuri wakiwa huko huko mkoani Songea..

Baadhi ya nyimbo walizofanya pamoja kama kundi ni kama vile

๐Ÿ‘‰๐ŸฟQueen
๐Ÿ‘‰๐ŸฟNakonda
๐Ÿ‘‰๐ŸฟCatherina
๐Ÿ‘‰๐ŸฟRoho mbaya ft pnc

mwaka 2004 kundi Hili la Muziki kutokea mkoani Songea lilivunjika na kubaki na msanii mmoja ambaye aliamua kuendelea kupambana na muziki akiwa kama solo Artist jina lake anaitwa G Luck

Msanii huyu kwa jina G LUCK alifanya nyimbo kadhaa akiwa kama solo Artist Nyimbo Hizo ni kama vile:

๐Ÿ‘‰๐ŸฟMPAKA SOO NA MOVIE YA KANUMBA (Ambayo tetesi zinasema kuwa inamlenga muigizaji lulu)

Lakini pia Msanii huyu aliweza kupata shavu katika matamasha ya FIESTA mwaka 2014 Baada ya kuwa mshindi wa "super Nyota" kutokea Mkoani Songea..
Mashindano ambayo yaliokuwa yanaandaliwa na "clouds Media Group"

Akiwa mshindi wa "Super nyota" msanii kutokea Mkoani "Songea"

Ambapo alizunguka kila mkoa kwenye matamasha ya FIESTA ilipopita ..

Ameshawai kutoa Ngoma yake iitwayo

Wa kwako je? ft Amini.

Kwa sasa msanii G Luck amegeukia upande wa siasa ambapo sasa ni mwenyekiti wa "UVCCM"

Kata ya Mshangano Songea mjini lakini pia Msanii Cammy boy kwa sasa ni muimbaji wa Nyimbo za injili katika kanisani linaitwa "RAGT" Mkoani Songea..

Hiyo ndio ilikuwa historia ya kundi Hili la Muziki kutokea mkoani Songea..

UKWAJU WA KITAMBO
0767 542 202
 
Historia nzuri, anaitwa Good lucky Mkoma, classmate wangu MAJIMAJI PRIMARY SCHOOL 2002.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ