Msanii gani alifanya uwe chizi wa muziki!

Msanii gani alifanya uwe chizi wa muziki!

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Kila shabiki kuna namna alianza kupenda muziki na hatimaye akajikuta hawezi kutoka tena!
Mi nakumbuka kwenye 90s mzee wangu alikuwa na music system ambayo alitoka nayo Russia na alikuwa akiplay ngoma kama Kesi ya kanga na nyingine za kikongo, muda ullienda baadaye nikawa nasikiliza wasanii mbalimbali hasa RTD.

Muda ulienda na msanii aliyefanya mikapenda zaidi muziki ni Mr 2 aka Sugu, huyu nimesikiliza na kukariri karibia ngoma zake zote kila album, toka Nje ya bongo, ndani ya bongo, millenia mpka muziki na maisha.

Zile rnb na rap za early 2000 ni kama zilikuja kukoleza, kiss fm na American Top 40 kulikuwa nyumban, early 2010 nimekuja kuuelewa zaidi muzidi wa pop na country, miaka yote sijaeahi iacha bongo fleva.

Mpaka leo nimejikuta kitu muhimu kwenye maisha yangu ni music, mwaka huu pekee nimesikiliza nyimbo zaidi ya 6k za wasanii zaidi ya 2k. Kifupi nimekuwa muumini wa good music haijalishi ni genre gani!

Ebu tuambie kwako ilikuwaje ukawa chizi wa muziki?
 
Nakumbuka miaka 90s kipindi hicho niko primary Bro alikuwa na redio yake ikiplay tape inajigeuza yenyewe nilitokea kuipenda san Ile redio hapo ndio ikawa mwanzo kuanza kusikiliza Old-school Hip-hop za kibongo hata za mbele ingawa lugha ilinipiga chenga nilipenda sana midundo yake

Rapa kama Method Man , Redman , Keith Murray, Eric Sermon, BigL, tulikuwa na albums zao z Tape pia Kwanza Unit, The Diplomat, Kala mashaka, KituSewer, Hapo ndio ilikuw mwanzo kupenda Hip-hop mpka Leo nasikiliza sana Ngumu
 
Back
Top Bottom