Msanii maarufu wa Marekani afariki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa filamu kutoka nchini Marekani, Kristoff St. John (52) amefariki dunia baada ya mwili wake kukutwa nyumbani kwake huko San Francisco, usiku wa Februari 2, 2019.

Msanii huyo maarufu ambaye alishawahi kuwekwa kwenye hospitali ya watu wenye matatizo ya akili baada ya kujaribu kujiua kwa bunduki, alipata umaarufu mkubwa kwa kuigiza kwenye filamu, ambazo alianza kujihusisha nazo akiwa na miaka nane tu.

Star huyo ameshawahi kuigiza kwenye filamu mbali mbali zikiwemo That’s My Mama, Wonder Woman, Roots, The Next Generation, na nyinginezo nyingi.

Mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijajulikana, ila polisi wa Francisco wameshuku huenda ikawa ni kuzidisha madawa, yaliyosababisha kifo chake.

Star huyo hivi karibuni alimchumbia mchumba wake Kseniya Olegovna Mikhaleva, na walitarajia kufunga ndoa ndani ya mwaka huu.

Zanzibar24
 

Mimi nilimfuatilia kwenye ile tamthilia ya 'The youngu and the restless' jamaa alikuwa anaongea kwa mapoz na alivyo HB, wakiwa na kina Vivica j Fox.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…