KWELI Msanii Rayvanny rasmi aondoka Wasafi

KWELI Msanii Rayvanny rasmi aondoka Wasafi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Hayawi Hayawi sasa yamekuwa, ilianza kama kamchezo kakuigiza kutokupeana support za kupostiana kati ya Rayvan na wasanii wenzake wawasafi lakini utetezi ukawa mwingi, Ikafuata mama yake Boss wa Rayvan kumkatia Behewa Rayvan huko Instagram yaan Mama Dangote kumunfollow Rayvan.

Zikaja Event zote kubwa za wasafi Ikiwepo EP ya FOA kutopostiwa na kijana huyo Shaban Mwakyusa Almaarufu kama Rayvan na Leo hii kaamua kukata Behewa kwenye Bio yake na kuondoa Taarifa iliyokuwa ikimtambulisha kama msanii wawasafi.

Inasemekana Rayvanny kaondoka Wasafi. Hii ni kweli?

1658127616724.png
 
Tunachokijua
Msanii wa WCB, Raymond Shaban Mwakyusa maarufu kama Rayvanny amethibitisha kuondoka wasafi na kufungua ‘label’ yake inayojulikana kama Next Level Music (NLM). Amethibitisha hayo Julai 12, 2022 kwenye mtandao wa Instagram, pia wakati alipohojiwa na vyombo vya habari wakati akionesha rasmi eneo lake la kufanyia kazi zake kama Rais wa label hiyo.

Rayvanny anasema kuwa malengo yake ya muda mrefu ni kuwainua vijana wengine wenye vipaji na kuweza kuwasaidia kama yeye alivyoweza kusaidiwa na Nassib Abdul (Diamond) na hivyo hana budi kutimiza yale yaliyokuwa malengo yake ya muda mrefu.

Pamoja na hayo amemshukuru Diamond aliyempokea, kumsaidia na kumkuza katika kipaji chake kitendo kilichofanya kwa yeye kujulikana zaidi kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wa pili, Diamond Platinum amekubali na amempongeza msanii huyo kwa kumtakia kila la kheri na mafanikio makubwa katika Label yake mpya na kwamba hakuna ugomvi baina yao kama maneno ya watu, wakidai kuwa anadaiwa na WCB jambo linalomfanya kuwa na ugomvi na boss wake.

Rayvanny ameondoka ikiwa ni takribani miaka 6 tangu ajiunge na kundi hilo lililomfungulia njia ya safari ya muziki.
Back
Top Bottom