Msanii Roma aishukuru serikali kwa jinsi ilivyoshughulikia suala la kutekwa

Socratic

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
568
Reaction score
308
Msanii Roma akihojiwa leo na clouds tv ameishukuru serikali kwa kunusuru maisha yake na kumrudisha uraiani.
 
Akihojiwa na watangazaji wa clouds fm kuhusu anapeleka wapi shukrani zake kuhusiana na tukio la kutekwa kwake.

Ameongea kwa msisitizo kwa kuishukuru serikali na vyombo vya dola kwa jinsi walivyoshughulikia suala lililomkuta.

NADHANI ROMA ANA SIRI NZITO SANA DHIDI YA WABAYA WA SERIKALI
 
kama alivyoahidiwa kuwa upelelezi kuhusu tukio la wao kutekwa unaendelea hivyo asilizungumzie, bado anaamini upelelezi unaendelea?

teh teh teh teh! asante sana Mwakyembe kwa kutumia akili kumzima huyu kijana na kumuungiza mjini
 
Pana tatizo hapa sio bure yani Roma ni kama ametoka kwenye ubatizo kabadilika sio yule hipop tena
 
Ni kweli, haki yake kuishukuru. Maana mwakilishi mmoja wa serikali aliahidi atapatikana kabla ya jumapili ya wiki na kweli akapatikana ijumaa wkt Kamanda Sirro kazi ilimshinda.
 
Aaaah anazinguwa nae ameshakuwa mwanasiasa porojo nyingi ameshindwa kutufumbua macho watanzania bwege huyo
 
Msanii Roma akihojiwa leo na clouds tv ameishukuru serikali kwa kunusuru maisha yake na kumrudisha uraiani.
Serikali kumrudisha uraiani??? Kwani SerikalI ndio iliyometeka?
 
Pana tatizo hapa sio bure yani Roma ni kama ametoka kwenye ubatizo kabadilika sio yule hipop tena
Amekuwa honest..
.nadhani wale aliomanishwa kuwa ni wema zaidi ya serikali amegundua ndio wabaya dhidi ya serikali na wanaweza kufanya lolote lile.
 


Hahahahahaha...na serikali imeshindwa kuwakamata hao wabaya...doh
 


Hongera kwa serikali ya Magufuli kushughulikia vema ishu ya Roma, wasanii wengine wamepata funzo pia kuwa serikali ipo na inawajali sana.
 
Atoke
Toka zake mnafikiki uyo,hana lolote anadanganya watanzania,Hakuna cha rap hapo ni taharabu tu,Kashindwa kusema alipelekwa wapi na kafanywa nini?kama kufa kupo tu hata usipokufa leo utakufa kesho.
 
behind of scene.. imefunikwa na pazia jeusi na zito
 
Huyu ROMA sioni haja ya kuulizwa chochote, yeye kashaamua kuwakumbatia watesji, wauaji na majangili kwa wanyonge.
 
Unamshukuru Nyani kwa kukutetea kwenye Kesi ya Ngedere.

Kwikwikwikwi!!!!

Huyu R.O.M.A siyo yule tena wa miaka ile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…