Msanii wa bongo movie Johari afunguka sifa za mwanaume anayemtaka kwa sasa

Msanii wa bongo movie Johari afunguka sifa za mwanaume anayemtaka kwa sasa

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
johari.JPG


STAA wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari' ameamua kuvunja ukimya wa muda mrefu baada ya kuweka wazi mwanaume ambaye anahitaji amuoe na sababu inayomfanya asijichanganye na mastaa wenzake.


Katika makala haya Johari amefunguka mengi, msome;

Mwandishi: Kwa nini mara nyingi hupendi kujichanganya na mastaa wenzako?
Johari: Ujue nina kampuni ambayo wakati wote nahitajika kuwepo hapo, na kama kujumuika, najumuika na wenzangu pale pa muhimu kama kwenye misiba.
Mwandishi: Tangu umeingia katika tasnia ya filamu kuna mastaa ambao mara nyingi wanawaweka wazi wapenzi wao lakini wewe haijatokea ni kwa nini?
Johari: Unajua kwa sasa ni kama dada wa mastaa, kitendo cha kuwaweka wazi wapenzi, wengi wanakuwa akili zao hazijakomaa, lakini najitambua na ninaelewa akili za wanaume, unamtambulisha leo kesho kakukimbia utakuwa unatambulisha wangapi?
Mwandishi: Mbona kuna tetesi kuwa Ray alikuwa anakukataza kumtaja hovyo wakati wengi wanajua ndiye mpenzi wako?
Johari: Sipendi kuzungumzia chochote kuhusu Ray kwa sababu kila mtu ana maisha yake na kwa nini anikataze?
Mwandishi: Kuna wanaume wengi huko nje wanapenda kukuposa lakini wanaogopa wakijua kuwa mastaa hawawezi kuposwa na watu wa kawaida, unalizungumziaje hilo?
Johari: Hapana! Kwanza kwa upande wangu nahitaji kuolewa na mwanaume wa kawaida ambaye anaweza kunijali na kujua thamani yangu na siyo wa kujibweteka, ajue kuchakarika na wala sichagui, maelewano tu.

Mwandishi: Mastaa wengi hawafanyi kazi mara nyingi wanategemea filamu pekee ambazo haziwasaidii, unalizungumziaje hilo?
Johari: Hilo hata mimi linaniumiza sana kwa kuwa mastaa wengi wa kike hawajitumi, asilimia kubwa ni tegemezi kwa wanaume ila ninachoona ni bora kuridhika na moja ya kwako kuliko elfu moja ya wenzako.
Mwandishi: Mara nyingi huonekani katika kumbi za starehe, kwa nini?
Johari: Kikubwa ni kazi na kukosa muda, pia sipendi kujichanganya sehemu kama hizo.
Mwandishi: Mna bifu lolote na Chuchu Hans?
Johari: Mmmh! Sina, sipendi zaidi kuzungumzia hilo, samahani.
Mwandishi: Muda unazidi kusonga mbele na karibia mastaa wengi wana watoto, vipi wewe unangoja nini?
Johari: Sidhani kama kuna mtu ambaye hatamani kuwa na mtoto, kwa upande wangu lazima nitafute baba mwema nitakayemzalia.
Mwandishi: Haya asante Johari.
Johari: Karibu tena.

Hapo kwenye red ndio kuna sifa anazotaka kwa mwanaume sijui kama na yeye ana amekamilika
 
alipokuwa mbichi alikuwa anataka mwanaume with a denzel face,body like tyson,styles like puff daddy and money like michael jordan.Sasa kadoda kashusha standards hadi substantial.Jua limekuchwa mama.
 
alipokuwa mbichi alikuwa anataka mwanaume with a denzel face,body like tyson,styles like puff daddy and money like michael jordan.Sasa kadoda kashusha standards hadi substantial.Jua limekuchwa mama.

Yani umenichekesha wewe mtu.Ila kuchagua sana mwishoni ndio huko
 
dunia imebadilika zamani wanaume walikuwa wanatutaka
Sasa eti sisi ndo tunawataka
Woooy my ribs jamani

By the way anamtoto hata mmoja!? Maana naona ni mwenzangu na mie jua linazama anawazia sifa za mwanaume anayemtaka
Is too late asichague tena akijitokeza hata kama le mutu we kamatia tuu
 
alipokuwa mbichi alikuwa anataka mwanaume with a denzel face,body like tyson,styles like puff daddy and money like michael jordan.Sasa kadoda kashusha standards hadi substantial.Jua limekuchwa mama.




Na kweli..hawa viumbe wengi wakiwa ktk 20's wanaringa sana!sahizi age imeenda ndo wanapata akili,safi sana
Nimecheki Wikipedia wanadai age anacheza 32,na ifika 36 hv hajaolewa nadhani vigezo vitazidi kupungua
 
oops!!!an open ended question...give me a blank cheque and i will feel in the figures.Make sure the cheque will not be dishonored.

Hahahaha you make me laugh again.I dont even know what are you talking about.What is cheque by the way?????
 
Hahahaha you make me laugh again.I dont even know what are you talking about.What is cheque by the way?????

cheque or check(american)=an order to a bank to pay a stated sum from the drawer's account, written on a specially printed form.
 
Hahahaha you make me laugh again.I dont even know what are you talking about.What is cheque by the way?????

The cheque is a nickname of Francis Cheka, the best Masumbwilaizing Prisoner in Tanzania....
 
Keshazeeka huyo ila ukimuuliza umri atakuambia ana miaka ishirini na tano wakati anakimbilia forty kama siyo foryy kamili
 
Yaani bidhaa yenyewe used masharti kibao hivyo?

Hii ndiyo inaitwa kuuziwa mbuzi kwenye gunia! demu mwenyewe mbaya masharti kibao wakati kuna watoto wazuri wanaokuja kwa uzuri wa ajabu! mwambieni ajioe mwenyewe hapat mtu hapa
 
Back
Top Bottom