Msanii wa Bongo Movies Aibuka na Kudai Ana Mimba ya Marehemu Mez B

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304


MSANII wa filamu za Kibongo, Doreen Reguna ‘Queen Magali' amefunguka kuwa kifo cha staa wa Bongo Fleva, Moses Mshagama ‘Mez B' ni pigo kubwa sana kwake kwani marehemu alikuwa ni mpenzi wake na alikuwa na mimba yake.

Akizungumza na gazeti hili huku akionesha sura ya masikitiko, Queen Magali alisema kinachomuuma zaidi ni kwamba, ujauzito wa marehemu aliokuwa nao, ulichoropoka saa chache baada ya kupokea taarifa za msiba huo.

"Nilipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, sikuamini, hata ndugu zake marehemu walinipigia simu, sikuamini hadi nilipompigia shangazi yake ambaye alinithibitishia msiba huo, hapohapo nikapata mshutuko, hali yangu ikawa mbaya hadi nikalazwa.

"Nashukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri.

"Kiukweli msiba huu kwangu umekuwa ni pigo kubwa, tulikuwa na mipango mingi na marehemu katika maisha yetu, alishanitambulisha kwa ndugu na jamaa zake wote wa karibu lakini nasikitika zaidi kwa kuwa nimechelewa kuhudhuria mazishi ya mpenzi wangu kutokana na kuzidiwa ghafla lakini nitafanya kila liwezekanalo ili nikaweke japo mchanga kwenye kaburi la mtu niliyempenda katika maisha yangu," alisema Queen Magali.

Baadhi ya wapenda ‘ubuyu' waliokuwa wakisikiliza mahojiano ya Queen Magali na mwanahabari wetu, walisikika wakihoji kwa nini mrembo huyo asianike uhusiano wake na Mez B kabla hajafariki lakini mwenyewe alidai walikubaliana uchumba wao uwe wa siri.

Mez B alifariki dunia nyumbani kwao Dodoma Ijumaa iliyopita ambapo alizikwa katika makaburi ya Wahanga wa Reli, Dodoma.

GlobalPublishers
 
Jamani hizi mimba nyengine mtihani watu hufurahia zina na kuzaa wana haramu ni aibu na laana
 
Anataka mali za marehemu hana lolote.Na walisema wafanye siri iweje sasa hivi anaanza kubwabwaja

Mh anatafuta kiki huyu???? Lakini bora aseme maana tb sugu watu wawe na tahadhari maana kisu kikali hiki kina baba fanueli wasijeingia mkenge
 
Duh hiyo mimba haina adabu kabisa, imesikia aliyeiweka kasepa na yenyewe ikasepa
 
valuu ni kali saana ukiunganisha na ukali wa jua la bongo movie lazima tamthiria hizi ziwepo
 
akili za bongo movies bhana wanazijua wenyewe...
 
Duh hiyo mimba haina adabu kabisa, imesikia aliyeiweka kasepa na yenyewe ikasepa
Mimba akili nyingi hiyo imeona tabu kulelewa na baba wengi ikaamua kumfuata mshua wake hukohuko kuzimu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…