Msanii wa filamu ‘aunty fifi’ ageukia huduma ya maombezi, anaombea watu wanapona…!!

Msanii wa filamu ‘aunty fifi’ ageukia huduma ya maombezi, anaombea watu wanapona…!!

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
aunty_fifi.jpg

MSANII mkongwe kwenye wa filamu na utunzi wa hadithi Aunty Fifi, ameuambia mtandao wa DarTalk kuwa baada ya kuokoa na kumjua mungu vilivyo, sasa ameamua kuanza kutoa huduma ya kuwaombe watu kwani tayari ameshafanya maombi kwa kijana mmoja ambaye alikuwa ameoza mguu na sasa amerudi katika hali yake ya kawaida.

Awali kabisa kijana huyo inadaiwa kuwa alitakiwa kwenye nchini India kwa matibabu lakini msanii huyo alitumia maombezi na kumtibu kabisa kijana huyo ambaye kwa sasa amerudi katika hali yake ya kawaida na kupona kabisa.

Mwandishi wa DarTalk, aliposikia taarifa hizo ndipo alipomtafuta Aunty Fifif ili aweze kufunguka zaidi juu ya ishu hiyo, ndipo aliposema kuwa ameamua kwenda kwenye utoaji wa huduma hiyo ili kuwafungua watu waliofungwa na magonjwa kwani anaamini uwezo aliopewa na mungu ndiyo unaofanya kazi.

“Kuna kijana mmoja alitakiwa kwenda India kwani mguu wake ulikuwa umeoza hivyo nikamtafuta kwa ajili ya kumfanyia maombi na kwa nguvu za Mungu kijana amepona na anaendelea na kazi zake kama kawaida na hii ni nguvu ya Mungu aliyonipa ili niweze kuwatibu watu wenye matatizo,” alisema.

Hata hivyo alisema kuwa aliamua kuokoka ili kuachana na mambo ya kidunia lakini kadri siku zinavyozidi kwenda uwezo wake unazidi kuwa mkubwa na tayari ameshafikia katika kiwango cha kumuombea mtu na akapona.
 
Nampa ushauri kama anakipaji cha kuombea na kuponya;
aanze ziara kwenye hospitali ya taifa muhimbili akishamaliza ahamie hospitali nyingine za wilaya nabaada ya hapo.. Aanze safari kufanya maombezi katika hospitali za mikoani

-itasaidia kupunguzia serikali mzigo mkubwa wa kutenga bajeti kubwa kwenye wizara ya afya na hivyo kiasi hicho cha fedha kuelekezwa kwenye nyanja zingine za maendeleo
 
duu umetoa kali,tuanze kuwapa iyo kazi akina mwingira,kakobe,mama rwakatare na wengineo na yule aliyeshindwa kumfufua mtu kanisani kwange nabii gwajima
 
maisha ni kujaribu popote..!
 
Kaunga kila siku nakwambia tuanze kazi yetu we unabaki kuhofia hofia tu!ona watu wanavokula bingo huku!'kwani ulikwamia wapi kufanya usajili?
 
Last edited by a moderator:
kama anatumika na Jehovah atabaki but if its otherwise she'll not finish one round!
 
duu umetoa kali,tuanze kuwapa iyo kazi akina mwingira,kakobe,mama rwakatare na wengineo na yule aliyeshindwa kumfufua mtu kanisani kwange nabii gwajima

Gwajima tunamfungulia ofisi chumba cha maiti!
 
Huyo mama mi namfahamu ni mtu wakigoma ni mpigaji tu ameona kwenye filamu amepwelea anageukia kwenye maombi watu wamaombi wamekua wengi na hawataki kuungana kila mmoja anafungua kijiwe chake ndio nini sasa(masilahi)sie yetu macho tutaona mwisho wake halafu kwani nilazima ukimponya mtu utangaze? mbona jesus yeye kaponya wengi na hakuwa namakeke kama wao matangazo ya Tv na radio nazile namba za simu za M'pesa naTigopesa zanini?
 
Nampa ushauri kama anakipaji cha kuombea na kuponya;
aanze ziara kwenye hospitali ya taifa muhimbili akishamaliza ahamie hospitali nyingine za wilaya nabaada ya hapo.. Aanze safari kufanya maombezi katika hospitali za mikoani

-itasaidia kupunguzia serikali mzigo mkubwa wa kutenga bajeti kubwa kwenye wizara ya afya na hivyo kiasi hicho cha fedha kuelekezwa kwenye nyanja zingine za maendeleo

I supporr u 100%
 
Ugumu wa maisha ndo kipimo cha akili, ukishindwa dili hili unajaribu dili lile - Piga dili mdada
 
kaunga kila siku nakwambia tuanze kazi yetu we unabaki kuhofia hofia tu!ona watu wanavokula bingo huku!'kwani ulikwamia wapi kufanya usajili?

namimi pia naomba unisaidie utaratibu nianze kutoa huduma hiyo
naona hali ya mwitikio kwa watz umekua mkubwa sana
 
Kaunga kila siku nakwambia tuanze kazi yetu we unabaki kuhofia hofia tu!ona watu wanavokula bingo huku!'kwani ulikwamia wapi kufanya usajili?

Mwanzo kila nilikuwa nikiona jina la snowhite napata picha ya dada mpole na mkimya wa kuvutia ,lakini kadri navyozidi kukusoma picha iliyobaki ni ya dada wa kuvutia tu lakini kwingineko mh...wameliwa...
 
Last edited by a moderator:
Dili hii. Mwenye namba yake anipe tuingie mkataba tuanzishe kanisa. Hela hizi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom