Msanii wa movie Mainda ageukia Muziki wa Injili

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
MSANII wa sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda' aliyewahi kutamba na filamu za kidunia, sasa ameamua kuimba muziki wa Injili ikiwa ni kumtukuza Mungu na kujiandalia maisha mema ya peponi.


Msanii wa sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda'


Akipiga stori na mwandishi wetu juzi, staa huyo aliyekuwa akiitwa Mwanaidi na kubadili jina baada ya kuokoka, alisema: Vijana siku zote tuna nguvu, tuna muda wa kutosha hivyo tunapaswa kumtumikia Mungu siyo mpaka tuchoke, tuzeeke au tufanye kwanza dhambi ikifika omega (mwisho) ndiyo unamkumbuka Mungu.


Mainda akiwa kwenye pozi


"Ninaimba kwaya tena sauti ya tatu, subirini muone ujio wangu mpya kwani nimeamua kumtukuza Mungu aliyeumba mbingu na nchi."
 

Attachments

  • mainda2.jpg
    30.6 KB · Views: 983
  • mainda 3.jpg
    41 KB · Views: 969
Hongera Ruth. Songa mbele usirudi nyuma. Wapo watakao kubeza hawatakosekana. Usiwaangalie, waombee nao wabadilike pia....
 
Nasikia siku hizi mziki wa injili unalipa kuliko muviz
 
kumbe hata mi naweza kuingia kwenye soka ingawa nina aka41
 
"Njooni kwangu nyote mnaoelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha" mwisho wa nukuu, ni maneno ya mwana wa Mungu aliye keti juu kuume kwa Mungu baba. Hongera Mainda
 
Hivi mbona Stara Thomas naye hasikiki kwenye nyimbo za Injili.....

Nasikia kaamua kurudi kwenye mziki wa kidunia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…