Msanii wa Nandy, Yammi atimkia kwingine! Aaga African Princess

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
African Princess Records inapenda kuwataarifu rasmi wadau wa muziki, vyombo vya habari, na mashabiki wote kuwa msanii wetu mpendwa Yasirun Yasin Shaban, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii Yammi, amehitimisha rasmi mkataba wa usimamizi wa kazi zake na lebo yetu ya The African Princess Label kwa makubaliano ya kirafiki na kwa manufaa ya pande zote mbili.

Katika kipindi chake akiwa chini ya The African Princess Label, Yammi ameweza kung'ara na kuonyesha kipaji kikubwa kilichowavutia wengi ndani na nje ya Tanzania. Tumeshuhudia mafanikio makubwa kupitia nyimbo zilizofanya vizuri, maonyesho ya moja kwa moja (live performances), na ukuaji wa umaarufu wake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Tunaamini kuwa lebo imetoa mazingira bora yaliyomwezesha Yammi kukua na kupevuka kisanaa, na tunafurahia kuona kuwa sasa amepata wawekezaji wapya waliovu- tiwa kuendeleza na kusimamia zaidi kipaji chake na kumsaidia kufikia hatua kubwa zaidi kimataifa.

Kuondoka kwake pia kunatoa nafasi kwa African Princess Records kuendelea na dhamira yake ya kuwainua wasanii wapya, kuwekeza kwao, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya muziki wa Tanzania na Afrika.

Tunamtakia Yammi kila la heri katika safari yake mpya ya muziki. Ataendelea kuwa sehemu ya familia ya African Princess, na mafanikio yake yatabaki kuwa sehemu ya historia yetu ya mafanikio ya pamoja.
Your browser is not able to display this video.
 
Yanawahusu wadaslamu sijaelewa wala siwajui.
 
KUSIMAMIA LABEL SIO SAWA NA KUSIMAMIA SHAMBA LA MAHINDI LA EKARI MOJA

KUNA MMOJA ANAMUOMBA BILIONI MOJA MWENZIE WAKATI HAJAWEKEZA HATA 50M KWA MSANII HUSIKA🀣🀣🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Label inahitaji uwe na hela,uvimilivu na upendo.Ngumu sana kuwekeza kwa husiye mjua,huku tu kwenye familia watu wanawakataa mpaka ndugu zao, japokuwa wanahela.
 

Pipijojo Ahamia Rasmi Kwa Nandy (The African Princess) – Mwanzo Mpya Wa Moto! πŸ”₯
Msanii chipukizi mwenye kipaji kikubwa, Pipijojo, anaendelea kupiga hatua kubwa kwenye tasnia ya muziki Tanzania baada ya kufanya mabadiliko muhimu katika safari yake ya kisanii. Baada ya awali kusimamiwa kimuziki na Chief GoodLove, sasa amehamia rasmi chini ya usimamizi wa Nandy, maarufu kama The African Princess β€” hatua inayotajwa kuwa mwanzo mpya wenye matumaini makubwa kwake.

Chini ya mwavuli wa Nandy, Pipijojo anatarajiwa kupata malezi bora ya kisanii, ubunifu wa hali ya juu, pamoja na fursa pana zaidi za kujitangaza ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Nandy, ambaye ni mmoja wa wasanii wanawake waliothibitisha uwezo wao kimataifa, anaamini katika kukuza vipaji vipya β€” na Pipijojo ni miongoni mwa majina yanayopewa nafasi hiyo ya kipekee.

Kwa mtindo wake wa kipekee unaochanganya ladha ya kizazi kipya na hisia halisi za muziki wa Bongo Flava, Pipijojo anaonesha wazi kuwa ana kitu tofauti cha kutoa. Mashabiki wake wana kila sababu ya kutarajia kazi zenye ubora wa hali ya juu, video za kuvutia, pamoja na collabo kubwa zitakazotoka chini ya uangalizi wa Nandy.

Hii si tu ni hatua ya kawaida ya kubadilisha menejimenti, bali ni game changer kwa Pipijojo β€” safari mpya inayoweza kumbadilisha kuwa miongoni mwa majina makubwa yajayo katika muziki wa Afrika Mashariki.

Chini ya Nandy Tayari Pipijojo kaachia wimbo wake wa kwanza "Siachiki" Wombo wa mapenzi Mzuri sana unaweza kuupata kwenye digito platfrom zote Duniani Unakaribishwa kuusikiliza, Kipaji hiki ni kikubwa sana , Hongela sana kwa nandy.

Endelea kufuatilia Pipijojo, kwa sababu hiki ni kizazi kipya kinachokuja kwa nguvu! πŸš€πŸ”₯
 

Attachments

  • Pipijojo - Siachiki.png
    1.8 MB · Views: 27
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…