ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
TAARIFA KWA UMMA
Ndugu MTEGANDA HUSSEIN almaarufu "MTEGANDA",
pichani, ametoweka jijini Mbeya tangu tarehe 25 December,2024 majira ya saa saba usiku.
MTEGANDA alikuwa jijini Mbeya kwaajili ya kushiriki onesho la muziki lililo kuwa likifanyikia TUKUYU MJINI.
Taarifa za awali zinasema aliibiwa/porwa vifaa vyake zikiwapo fedha na simu eneo la Uyole na alifika kutoa taarifa kituo cha Polisi na kuomba msaada wa kusafirishwa Dar es Salaam toka kwa maofisa wa jeshi la Polisi, jambo ambalo halikufanikiwa. Taarifa hiyo imetolewa na baadhi ya marafiki waliofika kituo kidogo cha Polisi kilichopo UYOLE ambapo walipewa maelezo hayo na maofisa wa Polisi waliowakuta kituoni wakati MTEGANDA akiwa amekwishaondoka kituoni hapo.
Hata hivyo, jitihada za kuendelea kumtafuta kupitia simu yake(ambayo bado inaita bila kupokelewa), na kuuliza katika ngazi ha familia yake kama alifanikiwa kurejea Dar zimefanyika bila mafanikio.
IIKIWA UTAMUONA MAHALA TAFADHALI, WASILIANA KWA NAMBARI ZIFUATAZO:
1.0767939845 (ALFA MSHANI)
2.🚨
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202