Shujaa Nduna
JF-Expert Member
- Sep 8, 2022
- 599
- 487
Nimeangalia clip yake ya maigizo inayoitwa(kazi na ngono)katika igizo hili limeanza vema lakini ktk kumaliza nadhani lina utata. Joti aliigiza kama binti mwenye elimu ya digrii anayetafuta kazi, lakini bosi akamtaka kimapenzi ili ampe kazi na aliposhindwa kugawa uroda bosi hakumpa kazi.
Joti akarudi nyumbani na kumsimulia mama yake na hatimaye yeye mama na mtoto wakaambatana kwenda ofisini. Na walipofika ofisini mama akamkamata roba bosi na kutoka naye nje halafu Joti akakalia kiti cha bosi ofisini na kuanza kutumia desk top kama mfanyakazi.
Sasa kwanini nasema amekosea, igizo lilipoanza lilikuwa linaashiria kufundisha kupinga unyanyasaji wa kingono toka kwa mabosi, rushwa ya mapenzi. Lakini limeisha kwa kuteka ofisi. Watalam mnisaidie hii ni sawa ktk kuwasilisha ujumbe?