Dunia ni ya ajabu sana.
Nadhani imefika wakati Vyama vyetu vya siasa viweke mbele Maslahi ya nchi.
Hasa Chama tawala. Kwa muda mrefu tewakilishwa na watunga sheria wenye uwezo mdogo sana kwenye maarifa na mipango ya miaka 200 ijayo mbele.
Matokeo yake mpaka sasa tunatumia sheria ,katiba, mipango ,elimu,tafiti na dira za wakoloni. Wakijadili jambo wanaangalia ushindi wa Chaguzi na kushika madaraka.
Naiomba CCM ya Dr.Bashiru na Polepole ikiongozwa na Mwanasayansi Mh. Magufuli ituletee watu walipitishwa kwa hoja zenye maono na sio umaarufu wa MTU kisanii sanii. Umaarufu utumike kuongoza vyama lakini sio Serikali wala kuwawakilisha wananchi.
Mihimili ya Dola ibaki kuwa ya watu wenye uwezo . Bila kufanya hivyo sio muda mrefu bunge litadharaulika sana kwani litaonekana kama muhimili wa wasanii na waimba twarabu tuu kuburudisha mihimili mingine iliyojaa watu wenye taaluma kubwa na watu makini.