Msanii wako bora wa mwaka 2021 kwenye Bongo Flavour

Msanii wako bora wa mwaka 2021 kwenye Bongo Flavour

torvic

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2016
Posts
3,978
Reaction score
9,841
Heri ya Chrismas na Mwaka Mpya!

Nianze kwa kusema mimi siyo shabiki wa Bongo flavour napendelea sana Hip Hop na Jazz lakini hapa acha nitoe hii tathimini yangu kwenye Bongo Flavour kwa mwaka 2021 ambao tumeacha siku chache kuumaliza.

Kwenye muziki wetu huo naona jamaa Marioo amefanya vema sana mwaka wote wa 2021 sana, almost ngoma zake zote alizotoa ndani ya mwaka 2021 ni kali na zimekuwa hit songs.

Nikiambiwa nimtaje msanii wa Bongo Flavour aliyefanya vizuri kwa mwaka 2021 basi ningesema Marioo.

Kwa upande wenu JF vipi? Mbali na huyo nilie mtaja, nani unaona amefanya vizurii zaidi mwaka 2021 kwenye Bongo Flavour?

Mtu ambaye amezingua kwa mwaka huu naona ni Rayvanny.. sisemi kama hajui, ila ajawa amshaamsha kwa mwaka huu.
 
P Mawenge hawezi kuingia hata top 30 ya waliofanya vizuri..

Au ni mshkaji wako unampigia pande kidogo humu jeifu[emoji3]?
Dah wala hata simfahamu ila nilisikiliza nyimbo yake anawasema wanaume legelege kwamba ni pisi kali kiukweli inachekesha na nyingine kashiriki inaitwa "fanya wewe" yupo vizuri bana
 
Dah wala hata simfahamu ila nilisikiliza nyimbo yake anawasema wanaume legelege kwamba ni pisi kali kiukweli inachekesha na nyingine kashiriki inaitwa "fanya wewe" yupo vizuri bana
Namjua fresh hupo P the Mcee..

But ndo hivyo,hawezi kumake top 30.

Kumbe hadi fanya wewe umeusikiliza??..nyimbo za wagumu hizi mtoto mzuri.
 
Back
Top Bottom