Msanii yupi wa Hip Hop nchini Tanzania unamkubali akiwa stejini?

Msukuma wa dar

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
1,160
Reaction score
1,195
Pamoja na changamoto zote ambazo mchizi anapitia, lakini akiwa kwa stage, jamaaa ana vibe flani la kukufanya usijutie kiingilio chako. Utampenda!!

Mchizi anakosa attention tu ya kufanya ngoma kali, ila jamaa yuko vizuri sanaa!!

Msanii mwingne wa Hip Hop mwenye uwezo km wa Chid ni Stamina Supermario aka Shorobwenzi aka Mr. Boniventure.

Huwa najiuliza ni kwanini wasanii wengine wanatuchukulia mashabiki poa, Mfano Fid Q. Mchizi anapenda sana kuongea ongea akiwa stage. Mchizi anaboa ila hajishtukiiagi tu.

Mwingine mzinguaji ni Nikki Mbishi, huyu jamaa anauwezo mkubwa wa ku-freestyle, ila akiwa stage ni uozo mtupu. Sjawai kumshuhudia akifanya hivyo kwny majukwaa makubwa Mf Fiesta.

Weusi
Hawa jamaa nao ni hakunaga tu. Show nyingi wanafanya kama kundi. Uwezo wa mtu mmoja mmoja ni zero.

 
Kiukweli Roma na Stamina ni wazuri sana kwenye kuchana live, wana pumzi na wanarap mstari kwa mstari (pumzi ipo), ni tofauti na wengine ambao hawamalizi maneno mfano Fid Q , binafsi huwa inaniboa ingawa nyimbo zake nazipenda, nadhani shida ni kuwa na pumzi ndogo.
 
Msanii anayeongoza kwa kuboa kwenye stage ni Jyma Natute.Sijawahi hata siku moja kumsikia akiimba live.Yeye ni mzee wa backup tu,alaf back up zenyewe anafanya kazi ya kufuatisha maneno machache na kujinyonganyonga kama nyoka tu.Juma Nature is very wack on stage
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…