BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI WA 'CRANE' YA NEW VICTORIA HAPA KAZI TU Mwanza, Tanzania.
Kuna taarifa iliyochapishwa na mtandao wa kijamii ikieleza kuharibika kwa mtambo wa kubebea mizigo (crane) wa meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kadhia hii imekuwepo kwa kipindi cha miezi miwili hivyo kuleta changamoto kwa wasafirishaji mizigo wanaolazimika kuwatumia wabeba mizigo kupakia au kushusha mizigo yao.
Kufuatia taarifa hiyo, Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:-
Ni kweli mtambo huo ulipata hitilafu ya kiufundi hali iliyosababishwa kuondoa ufanisi wa utendaji wake.
Baada ya tathmini, MSCL ililazimika kusitisha huduma za mtambo huo ili kupisha matengenezo yake. Katika kuitatua hitilafu hiyo, Kampuni ilifanya taratibu za manunuzi na kumpata mkandarasi mwenye sifa stahiki ambaye alianza kazi ya matengenezo mnamo tarehe 15 Oktoba 2024.
Shughuli za matengenezo zinatarajiwa kukamilika siku ya Jumamosi tarehe 9 Novemba 2024 na mtambo kuanza kazi siku ya Jumapili tarehe 10 Novemba 2024.
Aidha, pamoja na kuwepo kwa huduma ya mtambo huo melini, nafasi ya wabeba mizigo itaendelea kuwepo kwani baadhi ya wateja kulingana na aina ya mizigo yao wanahitaji huduma ya wabeba mizigo na sio mtambo wa 'crane'.
MSCL inawahakikishia wateja na wadau wote usafiri salama na wa uhakika wakati wote. Imetolewa na
Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Novemba 7, 2024
Pia soma:
- Meli ya MV. Victoria (Mwanza) haina crane ya kubebea mizigo zaidi ya miezi miwili, ni hujuma?
- Nimekosa huduma ya Meli ya MV. Victoria, inadaiwa haifanyi kazi wiki ya pili sasa, Mamlaka mbona mpo kimya?