“Msela” ni mtu wa aina gani?

“Msela” ni mtu wa aina gani?

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
#PilikaPilika: Kwa tafsiri rahisi “Msela” ni mtu wa aina gani?
1740416512332.jpg


#PilikaPilika #HainaKuchoka

Msela ni mtu asiyejali chochote. Apate chakula anafurahi. Asikipate anafurahi. Aibiwe anacheka tu. Apigwe anauliza "hujamaliza niondoke?" Ukimpeleka jela anakuuliza "kumbe hata hapa wanakula?" Umtishie kumuuwa anakuuliza "mbona umenikawiza?" Kiufupi msela hana ubaya na mtu
 
Msela ni mtanashati, msela mbishi kwenye utafutaji hakati tamaa kirahisi, msela ni mpambanaji msela chazaidi anaishi maisha yake haishi maisha ya mtu na anaweza akawa anavuta vitu lakini anajielewa kuanzia familia mpaka kazini.
 
Nawapa maana ya msela ss :-MSELA ni mtu ambaye haoni matatizo,hufanya anachotka na hajar watu watafikilia nn,yani ni mtu ambaye Yuko poa na kila mtu, anakuwa bize na mambo yake tu Hana Shobo,ila mtu huyooo ukimletea sizoo fasta anakuletea na yy, na sio tegemezi anaweza kuishi maisha yoyote Yale. Kimbelembele tunaweza tukasema Kama vile Eminem Yule ni msela, pia kuna mwingine unamkuta kimaisha yuko vizuri sana ila anaitikaeli za msela.
 
Mtofautishe kati ya:
1)Msela ngoto
2.)Msela mavi
3)Msela Mwanga
4)Msela Nondo

Ila Msela ni mtu asiye na makazi maalumu, na Msela ni msafiri yaani kifupi ni baharia(Sailor) ila wa nchi kavu.
 
Back
Top Bottom