Msemaji Mkuu wa Serikali atembelea wananchi

Msemaji Mkuu wa Serikali atembelea wananchi

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba ametembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) zilizopo Relini Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 16, 2024.

Makoba amepokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu ambapo wamezungumzia mambo mbalimbali ya kushirikiana na namna bora ya kujenga Taifa.

Snapinsta.app_455693830_1416707338993618_8857812465834858121_n_1080.jpg

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba ametembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) zilizopo Relini Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 16, 2024.

Makoba amepokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu ambapo wamezungumzia mambo mbalimbali ya kushirikiana na namna bora ya kujenga Taifa.
Sawa
 
Jiwe aliwaambia mwananchi kwamba "You are not free to that extent" kipindi hicho gazeti la mwananchi huwezi kulikuta mtaani saa nne asubuhi kwanzia hapo gazeyi la mwananchi nalo hufungia maandazi kama Jamvi la habari na Uhuru. Huyu nae ameenda kuwaelekeza nini cha kuandika na kipi kisicho cha kuandika. Siku hizi hatusomi tena habari za kiuchunguzi tunasoma habari za wanasiasa wakihutubiana na kusahau kuwahutubia wananchi kama alivyotanabiasha mzee Warioba. Hukuti mwanasiasa yupo jukwaani akisema "ndugu wananchi" bali husimama mbele ya wananchi kuwahutubia wanasiasa wenzao.
 
Back
Top Bottom