lanez
Member
- Apr 18, 2019
- 78
- 163
Tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, umalizike na Dkt. Magufuli kutangazwa mshindi, na jinsi alivyoanza kwa kasi na spidi 120, kila mtanzania alipata tumaini jipya kuelekea nchi ya ahadi. Pamoja na hayo aliibuka mtu mmoja, ambaye alimpinga Magufuli wazi wazi tena kwa nguvu zote, naye ni Tundu Lissu. Jinsi siku zilivyoenda, Mh Rais alizidi kupata umaarufu huku mtu anaye mpinga akiendelea kushambuliwa na viongozi wa CCM, wateule wa Rais na watu mbali mbali wanaomuunga mkono Mh Rais.
Kuonesha kuchukizwa na mtu anayempinga Mh Rais, huyu mtu akabatizwa majina mengi ikiwemo lile maarufu "msaliti ", . Watu wengi huu wimbo ulituingia, na kuanza kujiuliza huenda kweli Tundu Lissu kuna namna anafanya kurudisha nyuma jitihada za Mh Rais, licha ya hiyo Tundu Lissu aliendelea na msimamo wake ule ule. Swali likawa nani yupo nyuma ya Tundu Lissu ?, ni mabeberu kama inavyoelezwa , wananchi au yeye mwenyew kamua kupinga vitu asivyoamini.
Sasa baada ya Tundu Lissu kutangaza kuwania nafasi ya uraisi wa Tanzania , ambapo mgombea atakaye kuwa anachuana nae ni mh Rais Magufuli, basi kila mtu aliapata shauku ya kushuhudia mpambano huo. It is no doubt, kila mtu alijua hii mechi kabla haijaanza, Magufuli yupo mbele kwa magoli 5 kwa bila dhidi ya TL, mchuano huu ulichagizwa na kauli za kujiamini za Tundu Lissu, watu walitaka kujua nini kinamwamisha ?
Tangu siku anafika kulikuwa na shamra shamra za kumpoke, lakini wachambuzi wengi wa masuala ya siasa hawakuichukulia hali hiyo kama kukubalika kwake. Akatafuta wadhamin lakini bado hakudhihirisha kama bado anaungwa mkono. Siku chama chake kiazindua kampeni hapa Dar es salaam hakukuwa na mwitikio mkubwa sana, hata mimi nilihudhuria uzinduzi wao pale viwanja vya Tabata magengeni haikuwa kama ilivyo mikoani.
Kitu ambacho washindani wake waliendelea kubeza nguvu yake. Jamaa akaelekea mikoani, huko jinsi siku zinavyosonga, ndio jamaa anzidi kuwa na wafwasi wengi kila anapopita mpka hivi karibuni yale maneno ya washindani wake CCM ya mkutano hauna watu mara picha ya drone camera mara picha za 2015 yameanza kuisha. Hatimaye Tundu Lissu kadhihilisha ana nguvu na nitishio kwa uhai wa CCM, hii imeonekana baada ya mshindani wake mkuu mh Rais Magufuli kusema zile picha zinaunganishwa na za mwaka 2015.
Jambo lingine linaonesha CCM na watu wao wameanza kumhofia jamaa, ni press conference za mara kwa Mara za katibu mwenezi wa CCM, ambazo anatumia muda mwingi kumshambulia na kujibu hoja zilizotolewa na Tundu Lissu. Kutambua nguvu ya Tundu Lissu, imefanya msemaji wa ikulu, msemaji ofisi ya Rais wote kwa pamoja kujitokeza kumjibu Tundu Lissu.
Sasa, tujiulize kumbeza, kumkejeli na kumtukana mtu kama Tundu Lissu sio sawa na kuwatusi WANANCHI wanomuunga mkono , huyu ni mtu ambaye ana wafuasi wengi, kumbe ile kujiamini kote ni sababu ya wananchi walionyuma yake, kumbe ni sauti ya wasiosikika.
Mwisho, CCM wanatakiwa kurudi kweny blue print yao, waone kwa nini pamoja na yaliyofanyika lakin bado wananchi wanaunga mkono hizi harakati. Kwa sababu CCM hawakutegemea hili, ilipaswa wangalie jamaa anacho sema ndicho nao wakiseme, maana hamna namna. Lakini maajabu yake mgombea wa CCM na CCM wamekuwa wakijinadi kuongeza ndege licha ya wananchi kuoneshwa kutoridhishwa na haya mavitu. CCM iache kutukan huyu jamaa, kwani ni sawa na kutusi wananchi kwa ujumla 。