Msemaji wa hospitali ya KCMC akanusha taarifa za mgomo wa madaktari katika hospitali hiyo

Msemaji wa hospitali ya KCMC akanusha taarifa za mgomo wa madaktari katika hospitali hiyo

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
IMG_20210215_091702.jpg

Msemaji wa Hospitali ya KCMC Kilimanjaro, Gabriel Chiseo amekanusha taarifa zinazozunguka mtandaoni zenye madai ya kwamba madakatari katika hospitali hiyo wamegoma kufanya kazi kwa madai ya kukosa vifaa kinga (PPE) kutokana na ongezeko wa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa upumuaji.

Msemaji huyo amenukuliwa akisema:

"Madaktari kwenye ngazi zote wote wako kwenye majukumu yao ya kawaida, hakuna mwenye wazo wala mwenye nia yakufanya mgomo.

Kwenye vifaa vya PPE sio kweli kuwa tumevikosa ama kuna uhaba hata kama kuna vifaa tunavikosa sisi huwa kuna namna tunavipata na hili halijawahi kutokea katika hospitali ya KCMC.

Unapozungumzia mitungi ya gesi sisi tuna kinu cha kuzalisha mitungi hiyo, kwa siku mitungi ya Kilo 40 huzalishwa 400 na ile ya Kilo 50 huzalishwa 250 hadi 300 kwa siku, hivyo hakuna uhaba"
 
Hongereni sana kwa hili mjitangaze wengi hawajui kuwa mnazalisha. Hata watu binafsi wangeweza kuinunua.
 
Wale wapiga yowe ohhh mitungi ya hewa hospitalini haipo kanunueni yenu KCMC mkibanwa na mnachosema corona mwende na mitungi yenu ya hewa hospitali maruhuni nyie.
 
Madaktari wanawakimbia wagonjwa w covid-19 wakihofia maisha yao. Wagonjwa wenye changamoto ya kupumua kcmc ni wengi.
 
Wale wapiga yowe ohhh mitungi ya hewa hospitalini haipo kanunueni yenu KCMC mkibanwa na mnachosema corona mwende na mitungi yenu ya hewa hospitali maruhuni nyie
Ni half government half msamaria mwema (kanisa)
 
Hospitali ya KCMC ya mkoani Kilimanjaro kupitia kwa msemaji wake Gabriel Chiseo, imeweka wazi kuwa hakuna mpango wa kugoma kwa madaktari kwenye ngazi zote na wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.



KCMCA.jpg

Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro

Akiongea na Supa Breakfast ya East Africa Radio leo Februari 15, 2021, Gabriel Chiseo amesema, "Madaktari kwenye ngazi zote wote wako kwenye majukumu yao ya kawaida, hakuna mwenye wazo wala mwenye nia yakufanya mgomo" - Msemaji wa Hospitali ya KCMC Kilimanjaro, Gabriel Chiseo.

Aidha ameongeza kuwa, "Kwenye vifaa vya PPE sio kweli kuwa tumevikosa ama kuna uhaba hata kama kuna vifaa tunavikosa sisi huwa kuna namna tunavipata na hili halijawahi kutokea katika hospitali ya KCMC" - Msemaji wa Hospitali ya KCMC Kilimanjaro, Gabriel Chiseo.
 
Hongereni sana kwa hili mjitangaze wengi hawajui kuwa mnazalisha. Hata watu binafsi wangeweza kuinunua.
Haya endelea na nyodo zako za kumshambulia askfu Dr Shoo manake juzi ulipopa hizi fake news ukanyanyua makwapa na kumpiga vijembe.
Hapa KCMC madaktari wako kazini kuokoa maisha.
 
Haya endelea na nyodo zako za kumshambulia askfu Dr Shoo manake juzi ulipopa hizi fake news ukanyanyua makwapa na kumpiga vijembe.
Hapa KCMC madaktari wako kazini kuokoa maisha.
KCMC haimilikiwi na Shoo acha upotoshaji bali Serikali ni mbia mkubwa wa Hospitali hiyo
 
Wanaogopa kutoa ukweli wasiwe kama mganga wa Chunya
 
ndio maana nilikataa kusomea hilo kozi, hata wanangu sitaki wasome kozi ya kijinga kama hiyo, wanangu wote watasomea uchumi tu.
 
Back
Top Bottom