Msemaji wa Polisi, Misime asema: Mwandishi akikamatwa kama anahitajika kwenye uchunguzi zaidi wataendelea kumshikilia

Msemaji wa Polisi, Misime asema: Mwandishi akikamatwa kama anahitajika kwenye uchunguzi zaidi wataendelea kumshikilia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime akizungumza katika Kongamano la Wanahabari, Jijini Dar es Salaam, Juni 19, 2024 anaelezea: Jukumu letu ni kulinda mali za Watu na mali zao, wakiwemo Waandishi wa Habari, pamoja na hivyo muhimu ni kufuata Sheria zinazoelekeza.

Kuna miongozo na Kanuni juu ya kufanya nao kazi hata kama kuna mazingira ya hali ya usalama sio mazuri, pia tumekuwa tukiwapa maelekezo na mafunzo jinsi ya kufanya kazi katika mazingira tofauti.

Tunafanya makongamano na mijadala na Waandishi wa Habari, juu ya kufanya kazi pamoja, kuelezana mipaka ya pande zote mbili.

Hivi juzi mlisikia Rais aliunda Tume ya Haki Jinai na mojawapo ya yaliyojadiliwa ni jinsi ya Jeshi la Polisi kufanya kazi na Jamii.

Kutenganisha uhalifu na kuvuja taarifa binafsi
Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1970, inasema taarifa ambayo ni ya siri ambayo hautakwi kupita kwenye mifumo mingine ni kosa, ikitokea Mtu ameipata akaisambaza ni kosa.

Sheria ya Mitandao pia ukisambaza taarifa ambazo zipo kwenye uchunguzi, Mtu nashindwa kukwepa, anaingia kama ilivyo, sijui anatafuta followers.

Polisi tuna mchakato wa kupunguza sana uvujishaji wa taarifa, siku zijazo tutaona matokeo ya huo mchakato.

Haki ya Dhamana
Kuhusu Dhamana, zipo za Polisi zipo za Mahakama, Sheria inaeleza Mtu gani anatakiwa kupewa dhamana na katika mazingira gani na ni Mtu gani anatakiwa kupewa dhamana.

Mfano Uchunguzi wangu wa awali ukinionesha kwamba kupitia wewe naweza kufika sehemu fulani, lazima nitaendelea kuwa na wewe, tatizo Watu tunaenda kwenye Haki bila kuangalia mazingira ya uhalisia.

Pia soma
~ THRDC: Mwandishi aliyekamatwa akidaiwa kutumia nyaraka za siri bado hajapewa dhamana
~ Mwandishi aliyeandika tuhuma za RC Simiyu adaiwa kukamatwa na Polisi
~ Hii kamatakamata ya Waandishi wa Habari na ukimya wa Polisi, ni hatari kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari
~ Mwandishi aliyeandika tuhuma za RC Simiyu adaiwa kukamatwa na Polisi
 
Back
Top Bottom