Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
"Changamoto kubwa ni namna jengo lilivyodondoka maana watu wengi wamekamatika chini kwenye basement na jengo lilivyodondoka unaona upande mmoja jengo linaonekana na upande mwingine halionekani hivyo kifusi chote kimekusanyika upande mmoja sasa namna ya kukitoa kile kifusi kuwawahi watu na haujui mtu alibanwa upande gani." - Thobias Makoba - Msemaji Mkuu wa Serikali
"Kikubwa kinachoendelea sasa zoezi halijasimama tunaendelea na zoezi la uokoaji na leo ni kama siku ya tatu kimsingi wengine ni kama hatujalala na kuna vikosi, majeshi mbalimbali na wadau tumekuwa hapa usiku na mchana ili kuhakikisha wenzetu ambao wako chini iwe wako hai au ambao mauti imewakuta basi wote tunawatoa na kuwapa kile ambacho kwa hali yao wanastahili" - Thobias Makoba - Msemaji Mkuu wa Serikali
"Taarifa ya kusitisha uokoaji inapofika saa 6 usiku sijui imetoka wapi? Mimi nimekuwa hapa usiku na mchana hakuna siku wala saa ambalo zoezi hili limesitishwa. Unaowaona viongozi wetu na polisi pamoja na maafisa mbalimbali wanacho
fanya ni kubadilisha shifti tu na sio shifti ya kuacha kufanya kazi, ni shifti ya kutoka mtu anaingia mtu. Hapa vikosi vyote tunavyo, kikosi cha zimamoto ambacho ndio kinatuongoza kipo kikosi kizima hapa anasaidiwa na JWTZ, polisi wako hapa, mgambo wapo hapa, skauti wapo wamekuja kujitoa na wapo watu binafsi na taasisi binafsi ambao wanafanya hizi shughuli wamejitolea kuja hapa" - Thobias Makoba - Msemaji Mkuu wa Serikali
"Changamoto nyingine tunakwepa kutikisa huu upande unaoonekana kwa sababu ukitikisa upande huu unaweza kushusha jengo lote na hatutaki madhara yawakute wale walioko chini hivyo inabidi kutumia akili nyingi na uweledi mkubwa sio nguvu maana tunaona watu wanauliza mbona tunaona mashine, vifaa havitumiki niwaeleze hatuna changamoto ya kifaa wala rasilimali yoyote na ndio maana unaona maafisa wanakaa pembeni wanasubiri waitwe, na vifaa vyote viko hapa na Mhe. Rais amehakikisha vyote viko na ametoa kila kinachowezekana kwa amri yake watu wawe hapa lakini inabidi weledi na akili nyingi zitumike. Ukisema tufanye haraka, tutumie nguvu unaweza kusababisha madhara zaidi" - Thobias Makoba - Msemaji Mkuu wa Serikali
"Tangu jana baada ya kupata njia maana kuna mahali unapata njia lakini ni ndogo huwezi kumpitisha mtu hivyo kinachofanyika kwanza ni kuwapelekea gesi ya oxygen ili kuhakikisha kule chini wanaweza kupumua, pili maji wanapelekewa na watabibu wametushauri ili kurudisha nguvu haraka ni kupata glucose na madaktari na wataalamu wa lishe wako hapa wanawapelekea vitu" - Thobias Makoba - Msemaji Mkuu wa Serikali