Msemaji wa Serikali umedanganya; tuzo ya Nobel haijaenda kwa Raia wa Tanzania

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Prof. Gurnah aliyeshinda tuzo ya Nobel siyo raia wa Tanzania Kama serikali na viongozi wengi pamoja vyombo vya habari vilivyoripoti. Huyo ni raia wa Uingereza Mwenye asili ya Tanzania.

Msemaji wa Serikali hapaswi kuandika kwa kuangalia mitandao bali anapaswa kufanya utafiti. Haina haja kuwa na msemaji wa serikali na viongozi wa serikali wanaodanganya umma au kuripoti habari bila kujirizosha. Nadhani tuwe watu wakufanya utafiti.
 
wikipedia yake anasema ni mtanzania, ila ni raia wa UK

hatuna uraia pacha

cha ajabu website ya Nobel anaonekana yuko nchi zote mbili!!!
 
Mbona BBC pia wanasema ni Mtanzania, au mimi ndo sielewi.
Wamesema mwenye asili ya kitanzania na siyo mtanzania. Aliondoka Zanzibar 1960 kwenda uingereza Kama mkimbizi na alipata uraia wa uingereza. Tanzania hairuhisu uraia pacha hivyo ni wazi ilimlazimu kuukana uraia wa Tanzania.
 
Hatuna huo muda mkuu kwa maana watanzania tunaowajua huwa hawafuatilii habari wakishaambiwa. wakiambiwa Mike Tyson ni mtoto wa mzee Wassira utakuta ndio habari iliyozagaa kila mtaa...
 
Kule kuitetea CCM mitandaono ni Ukichaa kuzidi muokota makopo jararani. Maana huko jararani muokota makopo jararani aliwahigi kumuokota Paramagamba wa Kabudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…