Msemaji wa Serikali ya Kenya, Cyrus Oguna akutwa na Virusi vya Corona

Msemaji wa Serikali ya Kenya, Cyrus Oguna akutwa na Virusi vya Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Msemaji wa serikali ya Kenya, Cyrus Oguna amethibitisha kuwa na Virusi vya Corona baada ya kufanya vipimo na kupatikana na virusi hivyo.

Oguna aliwasihi wananchi wazidi kufuata maagizo wanayopewa na wizara ya afya na wachukulie virusi vya Corona kwa makini mno.

Mapema wiki hii, Rais Uhuru Kenyatta aliwaamuru mawaziri wote wasitoke nje ya jiji la Nairobi baada ya mawaziri watatu kupatikana na virusi hivyo.

Oguna amekuwa katika mstari wa mbele kupambana na virusi hivyo, huku mara kwa mara akiandamana na waziri wa afya Mutahi Kagwe katika kaunti tofauti.
Ni takribani zaidi ya siku mia moja tangu Kenya kusajili au kurekodi kisa cha kwanza. Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia afueni ya haraka.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 16,268 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 274, huku wagonjwa 7,446 wakithibitishwa kupona ugonjwa huo hatari.

Chanzo: RFI
 
Apone Haraka Sana Alijenge Taifa. Bado Kenya Inamuhitaji
 
Pole kwake.

Aje huku uhayani tumpe mshana.

Au apate juice ya mchanganyiko wa tangawizi, vitunguu maji, swaumu na asali kwenye maji ya moto.

Atafurahia
 
I don't know why you're minding for KE wakati kwenu hakuna report za covid.
 
Hongera sana kwa ujasiri wa serikali yetu kuendelea kuweka wazi, hii imetupea ujasiri kama wananchi na kuunga juhudi za serikali na kuwa kimoja, tusijichokee jameni, tuendelee kupima kupima kupima, nchi hii hatupo dhaifu.
 
I don't know why you're minding for KE wakati kwenu hakuna report za covid.
Report za familia yenu,wacha kiherehere cha kutaka kusikia mabaya kutoka kwa familia za wengine[emoji16][emoji16].

au vipi??
 
Hongera sana kwa ujasiri wa serikali yetu kuendelea kuweka wazi, hii imetupea ujasiri kama wananchi na kuunga juhudi za serikali na kuwa kimoja, tusijichokee jameni, tuendelee kupima kupima kupima, nchi hii hatupo dhaifu.
Mmepima watu millioni ngapi mpaka sasa mkuu?
 
mmepima watu millioni ngapi mpaka sasa mkuu???

Hapimwi kila mtu, kunao mpaka leo wanaona corona kwenye TV wala hawana habari nayo, hususan vijijini kule hawana habari kabisaa, sasa hamna haja kuwafuata unakwenda kuwapima.

Tunapima targeted individuals

- Waliohusiana au kukaribiana na waathirika
- Wahudumu wa mahoteli, wauguzi na madaktari n.k.
- Na yeyote mwingine mwenye ujasiri wa kutaka kuifahamu hali yake.
- Kuna baadhi ya hospitali ambazo zinapima corona kwanza kabla kukutibu chochote kilichokupeleka huko, sio kama nyie mnaosemekana kuwafukuza wanaonyesha dalili za corona hospitalini, eti hamtaki aibu ya kutajwa na mgnjwa wa corona, hivyo kila anayeumwa inabidi ajifiche ndani.
 
Hapimwi kila mtu, kunao mpaka leo wanaona corona kwenye TV wala hawana habari nayo, hususan vijijini kule hawana habari kabisaa, sasa hamna haja kuwafuata unakwenda kuwapima.
Tunapima targeted individuals
- Waliohusiana au kukaribiana na waathirika
- Wahudumu wa mahoteli, wauguzi na madaktari n.k.
- Na yeyote mwingine mwenye ujasiri wa kutaka kuifahamu hali yake.
- Kuna baadhi ya hospitali ambazo zinapima corona kwanza kabla kukutibu chochote kilichokupeleka huko, sio kama nyie mnaosemekana kuwafukuza wanaonyesha dalili za corona hospitalini, eti hamtaki aibu ya kutajwa na mgnjwa wa corona, Hivyo kila anayeumwa inabidi ajifiche ndani.
hizi taarifa za kuwafukuza umezitolea wapi? Halafu hujajibu swali la msingi,mmepima watu milllioni ngapi mpaka sasa?
 
Hizi taarifa za kuwafukuza umezitolea wapi? Halafu hujajibu swali la msingi,mmepima watu milllioni ngapi mpaka sasa?

Kwa mara ya kwanza nilidhani unajadili hoja kwa kutumia ubongo, kumbe nia ilikua zile ligi, haya subiri utajibiwa kiligi ligi kwa level yako.
 
Kwa mara ya kwanza nilidhani unajadili hoja kwa kutumia ubongo, kumbe nia ilikua zile ligi, haya subiri utajibiwa kiligi ligi kwa level yako.
Lakini swali si jepesi tu? Amekuuliza mmepima watu wangapi mpaka sasa?

Ni swala la kutaja idadi tu shida iko wapi?
 
Lakini swali si jepesi tu? Amekuuliza mmepima watu wangapi mpaka sasa?

Ni swala la kutaja idadi tu shida iko wapi?

Soma swali lako kisha linganisha na swali lake neno kwa neno, ukifaulu kupata tofauti nitakuona wa maana.
 
Ni hali ya kawaida kukutwa na virusi wa mafua hayo. Kubwa asiogope. Aendelee kuchapa kazi, huku akiendelea na matibabu na kuwalinda wengine wasiambukizwe.
 
Analogia Malenga,

Wakenya na mataifa mengine walibugi pale walipofunga nyumba za Ibada basi hakuna kingine na kuwajengea watu hofu shetani akapata nafasi ya kujimwambafai Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Rais Magufuli kwa swala hili la korona anakuwa rais no moja Duniani Kuamini na Kusimama Imara na kumtegemea Mungu ndie Muweza wa yote kama ni kufa hata malaria, kipindupindu,kansa na mengeneyo yote yanauwa lakini Alisimamia Imani Usiogope kwa kuwa Mungu yupo pamoja nasi na atatuvusha mpaka ukamilifu wa Dahali.
 
I don't know why you're minding for KE wakati kwenu hakuna report za covid.

It shows that we love our neighbour. In Tanzania we have nothing to record because there is no COVID 19 patients!!
Tanzania is the corona virus free country! This is proved by having no deaths! They once said that Tanzania can hide data but they cannot be able to hide deaths and its accompanying grief!! From that time they have been waiting to see mass deaths in the streets and in the community! To their disappointments there is none!

There is no parent who can allow his children to attend school without even a mask if he knows the deadly disease is still there!

Tourists are coming in great numbers because finally they have proved that Tanzania is the COVID 19 free state!! The reason behind is that we trusted God whole heartedly from the very begginig and leaders of other countries mocked us and mocked our God! For this case God decided to purify and glorify His mighty name by protecting Tanzania from corona virus infection!! This is the secret behind our success in the war against COVID 19! Unfortunately Kenya is one if the countries which mocked our President for believing God's protection!
 
Back
Top Bottom