Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Zanzibar), Hassan Khatib Hassan akielezea mfumo uliopewa jina la 'Sema na Rais Mwinyi' ambao anadai umesaidia kuwepo kwa #UhuruWaKujieleza kutokana na Wananchi kupata nafasi ya kumuuliza Rais maswali na kutatuliwa kwa changamoto zao
Anasema “Dunia yote mashirika yanasisitiza kuhusu uhuru wa kutoa maoni na sisi Serikali yetu imejitahidi sana, pia Rais Mwinyi anazungumza na waandishi wa habari na matangazo yanarushwa moja kwa moja.”
Ameongeza “Maadhimisho ya 30 ya #WPFD ni fursa nyingine kwa #VyombovyaHabari kutumia kufikisha ujumbe na malalamiko yao katika sehemu husika."