Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally hiyo Barua ya Kumfuta Kazi Kocha Mkuu Pablo unairusha lini? au Hasira zetu tuzianzie Kwako mjue mmetukera?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hasira zangu zinaenda kwa Watu hawa Wafuatao....

1. Mwenyekiti Mangungu
2. CEO Barbara
3. Kocha Msaidizi Matola
4. Meneja Rweymamu
5. Mratibu Abbas
6. Kocha Mkuu Pablo

Kuna Watu Wanne tajwa hapa ni 'Virusi Waandamizi' ndani ya Klabu ya Simba na ndiyo kwa 99% wametumika 'Kuihujumu' Simba SC kwa kutoa 'Siri' za Klabu na Mipango yote kwa Wapinzani wetu huku wakilipwa Mamilioni na Kampuni ya Tapeli iliyo na Ofisi zake Jengo refu kiasi Posta Mpya.

Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally tunawapeni hadi Jumatano muwe mmeshatangaza rasmi Kuachana na Kocha Pablo na kumpa Timu Kocha wa muda (mwenye Uchungu na Simba SC) ili azimalizie hizi Mechi za Ligi Kuu ya NBC zilizobakia.

Sijawahi kupandwa na Hasira kama Juzi.
 
Sidhani kuwa Simba ilihujumiwa jumamosi. Hizi lawama za Simba kushindwa zinapaswa kwanza ziwaendee wale wote waliofanya usajili kabla ligi haijaanza na wakati wa dirisha dogo. Kwa kweli hawakuitendea haki Simba kwa aina ya sajili walizofanya. Pili kushindwa kwa Simba jumamosi kuwe changamoto na funzo kubwa kwa bodi nzima ya Simba ili timu ifanye usajili wa maana kwa ajili ya msimu ujao.

Tuwe wakweli jamani Simba ilizidiwa kila idara uwanjani na bahati mbaya kwa Yanga lakini nzuri kwa Simba ni kufungwa tu lile goli moja. Iwapo safu ya ushambuliaji ya Yanga (Makambo na Mayele) ingekuwa makini nilikuwa naziona wazi kabisa goli 5 kwa 1. Sehemu ya kiungo ya Simba ambayo ndio mhimili kwa Simba kwa takribani miaka mitano sasa ilipotezwa kabisa na Yanga. Mbinu za benchi la ufundi la Yanga zilikuwa bora kabisa kuzidi zile za benchi la ufundi la Simba kwa kuanza na viungo wengi bila mawinga asili. Kitendo cha benchi la ufundi kushindwa kuudhibiti mfumo waliokuwa wanautumia Yanga kwa dakika zote 90 za mchezo ndio sababu kubwa ya Simba kushindwa mechi ile. Na kibaya zaidi kwa Simba ni aina ya maumbo ta wachezaji wao. Kwa wastani wachezaji wa Simba waliokuwa uwanjani jumamsosi walikuwa na maumbo madogo kulinganisha na wa Yanga kiasi ikitokea "one vs one" wachezaji wa Simba walikuwa wanapata sana shida.

Na hizi stori za Simba kuwa kama Al Haly, Orlando, n.k. ni vyema viongozi na mwekezaji wa Simba wakaachana nazo kabisa iwapo usajili wa mchezaji kama Adebayo tu unawatoa jasho. Sasa utashindana vipi na Al haly, Orlando, n.k. wakati Berekane tu wanakupelekesha kwenye usajili. Kama mwekezaji ameshindwa kuiboresha timu kwa kushindwa kusajili wachezaji wa maana basi ni vyema akaiuza timu au hisa zake kwa wawekezaji wengine wenye uwezo zaidi yake. Na hili halitakuwa la kwanza kwake kwani miaka michache tu iliyopita alishaiuza Sigara ikawa Singida United.
 
Kocha hamna kitu humo, mkabidhini matola amalizie mechi zilizobakia - huyo mspaniola aende zake - hatumtaki.

Uchebe pira tuliliona
Gomes pira tuliliona

Sasa huyu jamaa hamna kitu, timu imemshinda - wachezaji hawajitumi - aende.
 
kwenye 3 na 6 - kifupi sema tu benchi la Ufundi limeshindwa kazi - livunjwe.

Afu Takukuru waje kutusaidia kuangalia ni kina nani walisajili wachezaji maana kuna harufu ya rushwa - sasa mtu kama Mugalu itakuwa jamaa walikula cha juu.
 
kwenye 3 na 6 - kifupi sema tu benchi la Ufundi limeshindwa kazi - livunjwe.

Afu Takukuru waje kutusaidia kuangalia ni kina nani walisajili wachezaji maana kuna harufu ya rushwa - sasa mtu kama Mugalu itakuwa jamaa walikula cha juu.
Mugalu ni zigo la Samadi
 
Yaani kwa wachezaji wa Kigeni wa kubalia pale ni 5 tu tena kwa makubaliano maalum

1 Sakho - aache papara, muda wa kutoa pasi hatoi anakimbia kimbia hovyo tu - tutabaki naye ila akubali kujifunza, no gurantee ya number - ataipigania
2. Bwaya, huyu abakie kaonyesha uhai
3. Peter Banda - huyu abakie kwa umri wake ana room ya kujifunza zaidi - hakuna gurantee ya number aipiganie.
4. Chama tumvumilie kwa msimu mmoja atuonyeshe kitu - akishindwa atasugua benchi.
5. Inonga - hili jembe letu.

WENGINE WOTE MA PRO - FUKUZA - FUKUZA

Tafuta Mido mbili za hatari za kusaidiana na Mkude.
Tafuta Beki 2 za kati - zile za kazi kazi za kusaidiana na Inonga
Tafuta Striker moja matata sana ambaye pasi moja kaukamiza - ili atasaidiana na FAZA boko.

Mchezaji wa kuangalia - Mwanuke - ana kipaji anajituma, Simba wekeni jicho hapo.

Kwisha habari.

Simba oyeeeeeeee
 
Acha upuuzi wako. Kama umekosa kazi nenda kacheze pool table
Kwanini husemi nije nikukaze tu Uridhike kwani nayo ni Kazi pia na itanifanya niache vyema huo Upuuzi wangu?
 
Kocha apewe muda, bado mapema sana kumuwajibisha..kinachotakiwa ni usajili mzuriv
 
Kwenye issues za maana mnaleta mambo ya chupi na sindiria
 
Sidhani kuwa Simba ilihujumiwa jumamosi. Hizi lawama za Simba kushindwa zinapaswa kwanza ziwaendee wale wote waliofanya usajili kabla ligi haijaanza na wakati wa dirisha dogo...
Mkuu umeandika ukweli tupu.tulishasema sana haya
 
Yaani kwa wachezaji wa Kigeni wa kubalia pale ni 5 tu tena kwa makubaliano maalum

1 Sakho - aache papara, muda wa kutoa pasi hatoi anakimbia kimbia hovyo tu - tutabaki naye ila akubali kujifunza, no gurantee ya number - ataipigania...
Upo sahihi Ila hapo Kwa Duncan nyoni ondoa alishasepa kitambo

Labda km unamaanisha Peter Banda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…