Msemaji wa Simba SC Manara nifikishie haraka ‘ Ujumbe ‘ wangu huu muhimu kwa Kocha Aussems ili Nkana ‘ afe ‘ rasmi Dar

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwanza kabisa GENTAMYCINE nichukue nafasi kuwapa pole Wachezaji wa Simba SC kwa ‘ Kipigo ‘ cha jana kule Kitwe nchini Zambia ila pia niwapongeze kwa kupata goli muhimu sana la ‘ Ugenini ‘ ambalo naamini kama tutalitumia vyema na kwa haya nitakayoyaandika na kuyachambua hapa basi naamini Simba SC Jumamosi ijayo inatinga ‘ Makundi ‘ Klabu Bingwa Afrika.

Pili GENTAMYCINE niwape pole pia Wapenzi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yangu ‘ pendwa ‘ ya Simba kwa Kufungwa Kwetu kule jana ila nawaombeni tu msikate tama kwani nina uhakika wa 100% kama Simba SC itajipanga ndani na nje ya Uwanja na Sisi kwa umoja wetu ‘ tukashikamana ‘ kwa hali na mali katika maandalizi ya huo mchezo wa marudiano ‘ Mnyama ‘ anashinda tena mapema sana kama siyo mno tu.

OMBI LANGU MUHIMU KWA SIMBA SPORTS CLUB

GENTAMYCINE naomba mechi isichezewe Uwanja wa Taifa bali ichezewe Uwanja wa Uhuru ili wana Simba SC wote ‘ tuujaze ‘ ule uwanja kusudi uwingi wetu, makelele yetu na hata ule ukaribu wa Majukwaa na Uwanja pia uwe ni ‘ Kichocheo ‘ cha kuzidi ‘ Kuwachanganya Nkana Red Devils na tuweze ‘ Kuibuka ‘ Washindi.
Kuwapeleka Nkana Red Devils Uwanja wa Kisasa na mkubwa wa Taifa na ambao hauna Nyasi bandia kama ule wa Uhuru itakuwa ni kujipeleka Kwetu wenyewe ‘ Machinjioni ‘ Kufa kama siyo Kufariki kabisa kwani kwa jinsi nilivyowaona jana Nkana wakitiririka na kuserereka vile Kwao kuna uwezekano mkubwa tukicheza nao Uwanja wa Taifa itakuwa ni kama vile tunamtoa Nyoka katika barabara ya Vumbi na tunamleta katika Nyasi ambako ndiko sehemu yake ya Utawala na Kujidai Siku zote tokea ‘ Uumbwaji ‘ wake.


GENTAMYCINE naomba Kikosi cha Simba SC cha siku hiyo kibadilike na kiwe hivi kama ambavyo nakiweka hapa na baadae nitaelezea ni kwanini hasa ‘ Kiufundi ‘ zaidi:

Golini kama kawaida aanze Aishi Manula ( japo kuna muda huwa ananiudhi kwa kufungwa magoli yale yale )
Mbavu ya Kulia ( Beki mbili ) acheze Erasto Nyoni
Mbavu ya Kushoto ( Beki tatu ) acheze Asante Kwasi
Namba Nne acheze Paul Bukaba ( japo kuna mechi moja ya Ligi Kuu aliharibu ila kama akijengwa Kisaikolojia na akizidi Kuaminiwa na Kocha Patrick hakuna Beki mzuri wa Kati Simba SC kama huyu )
Kitasa / Libero ( Beki namba tano ) acheze Mchezaji wangu ‘ Kipenzi ‘ kabisa Mganda Juuko Murshid ( semeni mtakavyosema ila hakuba Beki wa Kati bora katika Afrika Mashariki na Kati hii kama huyu )
Kiungo cha juu ( Namba sita ) kama kawaida acheze Mdogo wangu mwenyewe Jonas Mkude
Shavu la Kulia ( Namba Saba ) acheze James Kotei ( ambaye Kimfumo atakuwa anacheza kama Kiungo )
Kiungo cha chini ( Namba nane ) acheze Hassan Dilunga
Namba tisa acheze Meddie Kagere
Namba kumi acheze ‘ Nahodha ‘ John Raphael Boko
Shavu la Kushoto ( Namba Kumi na Moja ) acheze Shiza Kichuya


Katika akiba ( Substitutes ) wawepo hawa akina Clatous Chota Chama Jr, Emanuel Okwi, Mohamed Ibrahim, Haruna Niyonzima, Pascal Wawa, Deogratius Munishi na Mohamed Hussein Tshabalala

Nimeweka hiko Kikosi hapo juu ‘ Kimkakati ‘ zaidi kwa kumtoa Beki Pascal Wawa ambaye jana ‘ alichomesha ‘ sana na isingekuwa umakini wa Yule Mshambuliaji ‘ imara ‘ wa Nkana na Nahodha wao jana Simba SC ‘ tungeyakoga ‘ mno Magoli.

Beki Pascal Wawa hata ‘ Usajili ‘ wake Simba SC sikufurahishwa nao japo naheshimu sana ‘ maamuzi ‘ ya Klabu Kumsajili. Ameshakwisha sasa hasa Kiumri halafu ni mzito sana Kugeuka ila tunamuona ni mzuri kwakuwa anapenda sana ‘ Kukaba ‘ kwa Kuvizia vizia ila kama Simba SC ikicheza na Timu yenye Washambuliaji ‘ Viberenge ‘ na ‘ Mbavu Mtu ‘ kama wa Nkana Red Devils au Azam FC ‘ tutatafutana ‘ Uwanjani.

Nataka Beki Mganda Juuko Murshid acheze kwakuwa ana ‘offer ‘ vitu vingi sana Uwanjani. Kwanza Juuko Murshid anauwezo wa Kucheza mpira wa Kazi Kazi, Pili Juuko Murshid ana uwezo pia wa Kucheza mpira wa ‘ Kihuni ‘ ambao kwa aina ya Wachezaji wa Nkana Red Devils walivyo na Kiherehere pamoja na Kimbelembele nina uhakika Juuko Murshid atamalizana nao mapema sana ( Najua Watu wa mpira kwa Lugha hii mtakuwa mmenielewa )

Nimeona mara nyingi sana ‘Chemistry ‘ ya Bukaba na Murshid huwa ni nzuri na humfanya mara nyingi sana Golikipa Manula awe Likizo ndefu kwani hawa Mabeki wanajua Kucheza ule mpira ambao GENTAMYCINE nautaka na naupenda hivyo kuifanya idara nzima ya Ulinzi Kukamilika.
Nimemtoa pia Kikosini Beki Mohamed Hussein Tshabalala kwakuwa japo ni mzuri kwa ‘ Kumiliki ‘ mpira ila ana ‘ Mapungufu ‘ ya Kimsingi la Kwanza ni kwamba yupo ‘ Slow ‘ sana na anapenda ‘ Kuupozesha ‘ mpira na Pili ni mzito Kupandisha ‘ Mashambulizi ‘ Vitu ambavyo huwezi Kuvikuta kwa Beki Mghana Asante Kwasi ambaye licha ya kuwa na vyote hivyo lakini bado pia anafunga.


Okwi na Chama napenda waanzie ‘Bench ‘ nikiwa na maana kwamba hizi ndizo ziwe ‘ Silaha ‘ zetu Kuu za kumaliza mchezo. Kumuanzisha pamoja Okwi, Boko na Kagere ni Kosa kubwa Kwetu ila ‘ Chemistry ‘ ya Boko na Kagere imekuwa ni nzuri mno na mara nyingi Okwi akiingia baadae huwa kunakuwa na Tija zaidi hivyo kupelekea Ushindi wetu.

Chama tayari hawa Wazambia wanamjua vyema na najua wana uhakika kuwa hata mchezo wa marudiano ataanza hivyo kama Kocha atamuanzisha baadae pamoja na Okwi huku akiwa tena amefanya ‘ mabadiliko ‘ katika nafasi ya Ulinzi wa Kati kwa kuwaanzisha Bukaba na Murshid nina uhakika tayari hii itakuwa ni ‘ Psychological Blow ‘ Kwao na itawachanganya sana na kutusaidia katika Ushindi.

MFUMO

GENTAMYCINE napendekeza Simba SC siku hiyo iwe isiwe tucheze kwa ‘ Kuvigawa ‘ Vipindi ili ‘ Kuwachosha ‘ na ‘ Kuwachanganya ‘ zaidi Nkana Red Devils. Katika Dakika 45 za Kwanza dakia 15 za mwanzo ‘ tushambulie ‘ sana kasha dakika 15 zingine ‘ tupooze ‘ mchezo ili kuwasoma tena na zile dakika 15 za mwisho ni ‘ mpela mpela / kushambulia ‘ kwa sana na nina uhakika hapa kuna ama Goli au Magoli tutapata / tutayapata.

Kipindi cha pili tubadili ambapo zile dakika 15 za mwanzo ‘ tupooze ‘ ili tuwaruhusu washambulie ili wachoke mapema kisha kuanzia dakika ya 15 hadi mwisho wa mchezo ya 45 waingizwe haraka akina Okwi na Chama kisha Timu ‘ ishambulie ‘ mwanzo mwisho ambapo pia hapa nina uhakika kuna ama Goli tutapata / Magoli tutayapata.

NIDHAMU

Pamoja na kwamba GENTAMYCINE nimekitaja hapo hicho Kikosi ila naomba sana siku hizi chache zilizobaki kabla ya Kucheza na Nkana Red Devils Wachezaji kama Jonas Mkude, John Boko pamoja na Juuko Murshid ‘ Wafundwe ‘ zaidi ili wasije ‘ wakatugharimu ‘ kwani wamekuwa na ‘ mapungufu ‘ yanayojirudia ya Kinidhamu japo kwa aina ya Washambuliaji wale viherehere / kimbelembele wa Nkana Red Devils hata kama Beki wangu ‘ Mtoto wa Mjini ‘ Juuko Murshid akipewa Kadi Nyekundu sitojali kivile kwani najua hatotoka peke yake bali atatoka na mmoja wa Washambuliaji hao wenye ‘ Sifa ‘ wa Nkana ambapo Juuko yeye ataenda Kupumzika zake Jukwaani ila nina uhakika huyo Mchezaji Yeye kuna mawili ama awekwe ICU Muhimbili au Wodi ya Mwaisela akisubiri ‘ matibabu ‘ zaidi.

FITINA

Hapa tusiwe ‘ Wanafiki ‘ na ukweli ni kwamba mpira wa sasa ni ndani na nje hivyo Simba SC tufanye yote ila tusisahau aina hizi mbili za fitina moja ikiwa ni ya ‘ Kuroga ‘ nay a pili ikiwa ni ile ya ‘ Kimafia ‘ zaidi najua hapa Kaka yangu Kassim Dewji ( KD ) atakuwa ananielewa vyema GENTAMYCINE pamoja na wale Watu wa mpira hasa huu wa Kibongobongo na wa huu wa Kiafrika.

Wa kwenda kwa Yule Mzee Wetu Morogoro na kwa Yule Bibi yetu Unguja waende mapema wakamalize ‘ Shughuli / Kazi ‘ kwa ‘ African Science ‘ yetu ila kwa wale ‘ Team Mafia ‘ wenzangu tujipange kuwamaliza Nkana Red Devils kuanzia Uwanja wa Ndege wa JNIA, wanapofikia, aina ya Usafiri wao, Maji yao, Vyumbani mwao hasa pale Uwanjani, barabarani na hadi katika Uwanja Siku moja yao ile ya Kuutumia Uwanja na Siku ya mechi yenyewe.

Kama pia hii mbinu itawezekana kutumika basi naomba ifanyike tafadhali. Kama kuna Kitu ambacho Raia wa Zambia huwa sit u kwamba hawakipendi bali pia ‘ wanakiogopa ‘ ni Milio ya Milipuko hasa ya Mabomu ( ya Machozi na siyo yale ya Kivita kabisa )

Simba SC tunaweza hata Kuongea tu na Police Tanzania hasa wale Watu wa FFU ili tuwapange Watu ‘ Kimafia ‘ na wajifanya wanafanya Fujo na wahakikishe wawe eneo ambalo Timu ya Nkana Red Devils imefikia kisha hao FFU wapige ‘ Mabomu ‘ kadhaa tena yale yenye milio mikali na mikubwa. Hii ifanyike Siku moja kabla ya mechi na hata Siku yenyewe ya mechi ila tu isiwe jirani sana na Hotel waliyoifikia ili wasije ‘ wakatushtukia ‘ na Kutushtaki CAF na ‘ ikala ‘ Kwetu. Umafia huu wa ‘ Kimchezo ‘ ufanyike ‘ Kiumakini ‘ mno.

Na mechi yenyewe ichezwe mchana wa Saa Nane (8) katika Jua Kali na siyo Saa 10 wakati ukali wa Jua unaanza Kupungua. Tusisahau ‘ Kijiografia ‘ Zambia maeneo mengi ni ya Baridi na hasa Mji wa Kitwe una Baridi hivyo kama Simba SC tukiwa ‘ wajanja ‘ tuwamalize Nkana Red Devils kwa Kucheza nao katika Jua Kali na bahati nzuri Jua la sasa hivi la Dar es Salaam linataka ‘ Sifa ‘ sana kwa Kuwaka hivyo nina uhakika Siku hiyo Wachezaji wa Nkana wataomba sana Maji ya Kunywa, Haja Kubwa zitawashika hovyo huku kil Saa wakiomba kwenda ‘ Kuoga ‘ kitu ambacho hakiruhusiwi wakati mechi ikiendelea hivyo kuwa faida kubwa Kwetu.

ANGALIZO

Japo GENTAMYCINE nimeandika mengi ila wana Simba Sports Club wenzangu tusijidanganye wala kujipa moyo sana kuwa tutawafunga au tumepita. Ukweli ni kwamba ‘ Kiufundi ‘ Nkana Red Devils wametuzidi baadhi ya maeneo lakini pia hata ‘ Kiuzoefu ‘ wa hii Michuano pia wametuzidi hivyo tusijiamini kivile na tukaenda na matumaini Kibao na matokeo yetu ‘ mifukoni ‘ mwetu tutakuja Kulia na Kuumbuka pale Uwanjani

Jamaa ‘ wanateleza ‘ vizuri sana na sehemu yao ‘ tishio ‘ hasa ni ya Kiungo na Ushambuliaji ambao ‘ Viungo ‘ Wao hawana mambo mengi kama Wetu ambapo Wao wakiipata tu ‘ wanaitupa ‘ kwa akina Binene na Kampamba ambao kwa jinsi wanavyotoka baru / wanavyokimbia utadhani wamefungwa ‘ Mota ‘ miguuni.
Na kinachoniogopesha zaidi ni kwamba Washambuliaji wa Nkana Red Devils wanajua sana Kupiga ‘ Miwa ‘ ( Kupiga Mashuti tena ya uhakika na yaliyotukuka kabisa ) hivyo umakini nao unahitajika sana vinginevyo Jumamosi ijayo wanaweza Kutufanya vibaya hapa hapa Dar es Salaam Kwetu kisha tukaanza sasa ‘ Kuwakoma ‘ Watani zetu Yanga SC ambao kama kuna Kitu ‘ wamebarikiwa ‘ nacho ni kujua kutupiga ‘ Madongo ‘ yanayouma Sisi Simba SC.


HITIMISHO

Nawatakia ‘ Maandalizi ‘ mema kabisa Simba Sports Club kuelekea huo mchezo na bado naamini na nina uhakika tena wa 100% kuwa Nkana Red Devils ‘ anakufa ‘ Jijini Dar es Salaam Jumamosi ijayo ya tarehe 22, December 2018 na Simba SC ‘ tutafuzu ‘ rasmi kuingia katika ‘ Makundi ‘ Klabu Bingwa.

Msiogope na wala msinyong’onyee bali mjiamini kabisa na GENTAMYCINE nimesema Simba SC ‘ tutafuzu ‘ Makundi ila niwaombe sana Mashabiki, Wapenzi na Wanachama wote wa ‘ Mnyama Mnyamani ‘ ( Simba Sports Club ) hakikisheni mnajipatia ‘ Tiketi ‘ zenu zikianza Kuuzwa na ‘ Muujaze ‘ Uwanja kwa rangi Nyekundu na Nyeupe tupu.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Simba Sports Club
Mungu wabariki Washabiki, Wapenzi na Wanachama wote wa Simba Sports Club popote pale walipo duniani
Mungu mbariki sana na mno GENTAMYCINE
Mungu usisahau pia ' Kuwalaani ' vibaya mno na sana wale ' Washamba ' wote wa Kitanzania watakaoishangilia Nkana Red Devils Uwanjani. Tena ' Uwalaani ' kweli kweli Baba Mungu.


Nawasilisha.
 
Ujumbe wako mkuu Gentamycine nimeshaufikisha kwa kocha ila umenipa kazi ngumu ya kumtafta mkalimani ili amsomee huu ujumbe alaf amtafsirie kwakua mimi Ung'eng'e Nikiongea napatwa na kwikwi, mfano neno kama jua kali la saa8 cjui hta nianze vp kumwambia
 
Inshallah Mkuu binafsi sijaelewa sub anayofanya kocha, jana Dilunga anaingia dk ya 87? Kati ya Okwi na Boko nani alipaswa atolewe mapema?
 
Kwa kawaida mkuu huwa unaandikia gazeti gani makala zako!?
 
Ndugu umeandika mengi ya msingi ila umeongelea washabiki Wa simba pekee vipi kuhusu washabiki Wa timu zingine hawapaswi kufika pale shamba la bibi? Naomba umshauri Manara aweke na nafasi yetu sisi ndugu zenu Wa karibu "YOUNG AFRICANS FOOTBALL CLUB" The Citizen Team" sababu tutakuwepo pia tukipiga makelele ya hapa na pale kuwapa nguvu wachezaji watakaokuwa wanacheza siku hiyo.
 
Hakika nakuunga mkono ,pia kikosi chako ulichokipanga nimekibariki
 
Tukupe Timu ya Taifa?....
 
Kikubwa umeheshimu uwezo wa Nkana the Red Devils. Wasiojua mpira wanadhani mtapita kama kwa Mbabane.

Katika jitahada za kutafuta goli moja, backline inaweza kuwa exposed na Nkana wakatumia counter attacking.

Naiona sare ya aina yoyote.
 
Inshallah Mkuu binafsi sijaelewa sub anayofanya kocha, jana Dilunga anaingia dk ya 87? Kati ya Okwi na Boko nani alipaswa atolewe mapema?
Kiufupi Simba hatuna kocha, tuwe wakweli. Huwezi kuelewa kwanini viongozi walimuondoa Pierre na Masoud.wakamleta huyu.

Kwanza kwa game plan yake na Nkana.anaonekana hakuangalia video za Nkama au he is technically inept. Hakutakiwa kufunguka kiasi kile.

Alitakiwa ailinde.sana.defence yake ambayo inaonekana haina pace kabisa, na kwa medhi ya juzi ndio tumeona jinsi gani kumtegemea Wawa katikati tunakuwa tunacheza kamali.
 
Kwa kawaida mkuu huwa unaandikia gazeti gani makala zako!?

Sina Gazeti lolote ninaloliandikia zaidi tu ya Kupenda Kuandika hapa ' Makala ' zangu nikiamini kuwa huwa zinasomwa na Watu makini ( Great Thinkers kama Wewe ), ispokuwa hao wenye Magazeti yao pamoja na ' Blogs ' mara nyingi hupenda Kutumia haya ' Maandiko ' yangu japo ambao huwa wananifanyia ' acknowledgement ' ni Wachache ila wengi Wao hujifanya kama hizo ' Makala ' wameziandika Wao. Mifano ya hii ipo mingi sana kama na Wewe ni Mfuatiliaji mzuri wa Websites / Blogs mbalimbali utakutana nayo huko.
 

Hapo kwenye Simba SC haina Kocha mzuri nitakupinga tena kwa 100% zote na nadhani unatakiwa ujibiidishe mno katika Kuusoma mfumo mzima wa Kocha Aussems. Nawaheshimu Makocha wote wa Simba SC hadi huyo uliyemtaja ila kwa sasa Kocha Patrick ameweza kutengeneza ' Chemistry ' nzuri ya Wachezaji na hata Wachezaji nao wanamuelewa isipokuwa ' Changamoto ' ndogo ndogo hazikosekani.

Kisaikolojia nimegundua Kitu kuwa umeathirika na jinsi Yanga SC wanavyoshinda na labda kuona kwamba Simba SC tumeachwa au tunaachwa pasipo hata kuangalia ' Factors ' zingine ambazo ni muhimu sana kama siyo mno. Una uhakika gani kwamba Yanga SC watashinda tu Kila Siku? Una uhakika gani kama Simba SC hatutashinda mechi zetu zote? Acha Uwoga Mkuu na Mshindi hupatikana mechi ya mwisho na bado nina uhakika tena hadi Kiburi kuwa Simba SC msimu huu tunakuwa Mabingwa tena.

Ukija na Hoja kwamba Simba SC ifanye haraka Kumtafuta Kocha Msaidizi hapo nitakubalina nawe bila matatizo yoyote yale.
 
Mechi ngumu sana hii!

Ni kweli ila kama ' tutajipanga ' vyema na ' Kimkakati ' ndani na nje huku tukiwa na Umoja wetu na Mshikamano baina ya Mashabiki, Wapenzi na Wanachama hadi kwa Viongozi nakuhakikishia Mkuu Jumamosi ijayo tarehe 22, December 2018 Nkana Red Devils ' anakufa ' tena mapema tu hapa hapa Dar es Salaam.
 
Nashauri wewe uwe Kocha msaidizi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…