Mkuu
GENTAMYCINE mimi nakubaliana nawe kwa % kubwa kwenye uzi huu.Ila kuna baadhi ya mapopoma hawatakuelewa na wala hawatanielewa mimi kuhusu hili.
1.Kama kuna watu wananikera ndani ya kikosi cha Simba ni Nikolaus Gyan,Aishi Manula na John Boko.
Huyu Gyan ana "pasi zisizo macho" za kutosha,akipanda mbele si mwepesi wa kurudi nyuma kwenye nafasi yake,na ana papara kibao.Na wale 'viberenge' wa Nkana hawahitaji mtu aina yake.Ndo maana kocha Patrick Aussems alisikitika sana baada ya Shomari Kapombe kuumia.
Tatizo la Aishi Manula ni kutojirekebisha na hivyo kuruhusu magoli ya aina ile ile,"miwa ya mbali".Gwiji Mohammed Mwameja alizungumza kuhusu tatizo la Manula siku chache kabla Simba haijaenda Zambia.Na Mwameja was 100% right,Manila alifanya makosa yale yale Zambia.Kiukweli,tangu zamani mimi huwa namwona Deogratius Munishi "Dida" kuwa ni bora kuliko Aishi.
Kapteni John Bocco sijui amekuwaje tu siku hizi?Anaweza kupata nafasi 9 nzuri za wazi,akaitumia 1 tu kwa usahihi.CAF Champions League haitaki huo uzwazwa.Unadhani mastraika wa Nkana FC Bwalya na Kampamba wanaweza kufanya ujinga huo?vipi wale wa Esperance?..kosa nafasi 2 basi,ile ya 3 fanya kweli!
Naomba nimwongeze na huyu Shiza Kichuya.Siku hizi anabutua tu akiwa karibu na lango utafikiri amepewa tenda ya kuangusha madafu kwa mashuti!Niliwaona hata strikers wa Mbabane Swallows hawapigi 'mipigo' ya Shiza Kichuya,ingawa walifungwa vya kutosha.Walikuwa wanapiga kimo cha mbuzi! Na siyo kulenga taa za jukwaani...Michuano hii ina nidhamu yake.
2.Kuna kitu watu hawataki kukielewa kuhusu Simba SC vs Nkana Red Devils,hasa vyura kutoka majalala sijui ya wapi vile...Simba haijawahi kuifunga Nkana pale Kitwe,wala Nkana hajawahi kuifunga Simba hapa Dar.Vyura wanatambua hili?
Simba imekuwa ikitolewa na Nkana kwa tofauti ya magoli tu!Siyo kufungwa Dar.Na hata Nkana wanajua kwa kuishia kushinda 2 - 1 Kitwe,wana kazi ya ziada Dar (hawakutegemea kukomea ushindi huo hafifu). Maana kwa miaka yote pale Kitwe wamekuwa wakishinda zaidi ya magoli 3,na hiyo imekuwa ikiwabeba....leo wanakomea 2 - 1?hata wao wanajua kazi ipo.
Naamini MNYAMA LAZIMA ATASHINDA ndani ya Dungeon yake!