Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
"Bodi ya Wakurugenzi, Sekretarieti, Benchi la Ufundi na wachezaji wa klabu ya Simba, wanawaomba radhi Wanachama na Washabiki wetu kwa matokeo ya leo (Jana).
Tumeumia sote na tunawaomba mjue hii ni mechi ya nne tu.
Tutafanya maamuzi sahihi bila pressure kwa maslahi makubwa ya timu na klabu, tunawaomba mtulie katika kipindi hiki". Haji Manara
NB: Tahadharini sana viongozi wa Simba kwa hayo maamuzi ambao mnayotarajia kuchukua, yasije yakaigharimu timu msimu huu 2018/19.Tufikie wakati tuheshimu matokeo ya mpira wa miguu, hakuna kocha anayependa matokeo mabaya katika timu yake, kufungwa ni sehemu ya mchezo, na huenda tukafanya makosa tutafukuza makocha kila siku ilhali pengine wachezaji wetu kushindwa kufanya kile walichoelekezwa.
Wachezaji wetu wanatakiwa kujituma na kujitolea kwa ajili ya timu na kuongeza umakini zaidi na kutumia nafasi zinazopatikana uwanjani vizuri.
Vile vile viongozi acheni kusikiliza kelele za mashabiki na kutaka kufanya kila wakitakacho mashabiki, lazima muwe na msimamo aisee, ikiwa Real Madrid au Man United inafungwa iweje Simba? Football ina results zake hivyo tuache kwenda uwanjani na matokeo mfukoni hiyo haipo, kwani hata mpinzani wako naye anajiandaa kukabiliana.
...........Ghazwat ........