Msemaji wa Simba: Tutafanya maamuzi sahihi bila pressure kwa maslahi ya Timu na Klabu

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
"Bodi ya Wakurugenzi, Sekretarieti, Benchi la Ufundi na wachezaji wa klabu ya Simba, wanawaomba radhi Wanachama na Washabiki wetu kwa matokeo ya leo (Jana).

Tumeumia sote na tunawaomba mjue hii ni mechi ya nne tu.

Tutafanya maamuzi sahihi bila pressure kwa maslahi makubwa ya timu na klabu, tunawaomba mtulie katika kipindi hiki". Haji Manara

NB: Tahadharini sana viongozi wa Simba kwa hayo maamuzi ambao mnayotarajia kuchukua, yasije yakaigharimu timu msimu huu 2018/19.Tufikie wakati tuheshimu matokeo ya mpira wa miguu, hakuna kocha anayependa matokeo mabaya katika timu yake, kufungwa ni sehemu ya mchezo, na huenda tukafanya makosa tutafukuza makocha kila siku ilhali pengine wachezaji wetu kushindwa kufanya kile walichoelekezwa.

Wachezaji wetu wanatakiwa kujituma na kujitolea kwa ajili ya timu na kuongeza umakini zaidi na kutumia nafasi zinazopatikana uwanjani vizuri.

Vile vile viongozi acheni kusikiliza kelele za mashabiki na kutaka kufanya kila wakitakacho mashabiki, lazima muwe na msimamo aisee, ikiwa Real Madrid au Man United inafungwa iweje Simba? Football ina results zake hivyo tuache kwenda uwanjani na matokeo mfukoni hiyo haipo, kwani hata mpinzani wako naye anajiandaa kukabiliana.

...........Ghazwat ........
 
Fukuzeni na viongozi waswahili kama kina Manara! Tarehe 30 Mambosasa ahakikishe kila shabiki wa mkia anakuwa na askari wake la sivyo vile viti vitapata tabu sana! This is Simba bhana.........
 
NDUGUUU YANGUU SHIDAA SIOO MASHABIKI SHIDAA LUGHAA WACHEZAJI WANAMTAKA MASOUD MIKOAN PIA SABABU B RAHISI KUELEWA ANACHOONGEA NAWATAKIA HERI NASIKIAAA

OMBAOMBAA NDIE ANAONGOZA LIGI SINAHAKIKA LAKINI
 
Fukuzeni na viongozi waswahili kama kina Manara! Tarehe 30 Mambosasa ahakikishe kila shabiki wa mkia anakuwa na askari wake la sivyo vile viti vitapata tabu sana! This is Simba bhana.........
HIIGAME IMEAHAIRISHWA MKUU AWAJASEMA LINI LAKINI SIO 30 TENA
 
Fukuzeni na viongozi waswahili kama kina Manara! Tarehe 30 Mambosasa ahakikishe kila shabiki wa mkia anakuwa na askari wake la sivyo vile viti vitapata tabu sana! This is Simba bhana.........
Hahahahaha
 
NDUGUUU YANGUU SHIDAA SIOO MASHABIKI SHIDAA LUGHAA WACHEZAJI WANAMTAKA MASOUD MIKOAN PIA SABABU B RAHISI KUELEWA ANACHOONGEA NAWATAKIA HERI NASIKIAAA

OMBAOMBAA NDIE ANAONGOZA LIGI SINAHAKIKA LAKINI
Labda
 
Wampe Djuma ambaye ndiye anaonekana akiwepo timu inashinda....mpeni chake mzungu wa watu ila mjue unafiki haufai kabisa.....mkishindwa fukuzeni wote halafu muwe mnajua kuwa kocha mkuu ndiye anayeteua kocha msaidizi ili kuondoa migogoro sio huo utaratibu wenu wa kishamba.
 
Mikia FC.
 
Toeni takataka huyo kocha msaidizi,ndiye anayeigawa timu isifuate maagizo ya kocha mkuu,makocha wawili wa kigeni wameondoka kwa sababu yake na huyu wa tatu anamtengenezea mazingira afukuzwe ilia apewe yeye timu,huyu ndio tatizo kwani anawagawa wachezaji kuwa wasimsikilize kocha mkuu,litoeni lipuuzi hilooooooooooo
 
Sikuona sababu yoyote ya Uongozi wa Simba kutokumuongezea mkataba bwana Pierre Lechantre.Narudia hakukua na sababu yoyote.Moo asipopata mwarobaini wa viongozi waswahili pale klabuni atapata tabu sana.
 
Kama wameleta mzungu kwanini wasingemwacha aliyekuwepo na kuwapa ubingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…