Jamaa alikuwa mteja wa kitimoto eneo flani wakati dini yake hairuhusu.
Siku ya siku akachukua baby wake mpya akaamua kumpeleka ili apate kitimoto, baby mpya akijua hapo walipokwenda jamaa hakuna namna anaweza kuwa keshawahi fika kwani dini yake hairuhusu.
Sasa walivyofika tu eneo la tukio, mpishi kwa bashasha kabisa akamkimbilia mteja wake wa siku zote na kumuuliza " Boss kama kawaida?"
Aisee kilichotokea hapo , ni kwa mpishi kukumbana na suluba ya aina yake toka kwa mteja wake mzoefu.
Tuwe makini na kauli hii, inaweza zua yasiyotabirika.