Mshahara laki mbili mkoani, au nijilipue Dar?

Jamaa hukumuelewa , Anamaanisha mshahara wa laki 2 siku hizi si chochote hata kama unalipwa huwezi fanya lolote la maana kwenye Dunia hii ya Leo
 
Nilipataga kazi ya u meneja kampuni ya Star Oil ya Mo (METL) Mshahara eti 450,000

Hapo na Shahada yangu ya engineering

Hii nchi acha tu
 
Komaa mkoani kwanza angalau kwa miezi 7-8 huku ukijibana kusave kila senti.


Tumia muda wako wa ziada kujifunza high-demand skills online.


Ukiamua kuja Dar, make sure uwe na angalau kiasi cha kukuvusha 3 months runway na uwe umeshafanya interviews kadhaa.
 
Nashukuru sana
Unaweza kunisaidia kunitajia high demanded skill ambazo natakiwa kukomaa nazo kwa sasa?
Ili iwe rahisi kuzifahamu?
 

Kwamba Mimi nimejipata sio😃
Mimi nazungumzia ukweli iwe umejipata au haujajipata.

200k kwa maisha ya sasa huwezi uita mshahara.

Hao wote uliowataja wanatakiwa walipwe mishahara na sio hayo malipo kama posho.
 
Kwamba Mimi nimejipata sio😃
Mimi nazungumzia ukweli iwe umejipata au haujajipata.

200k kwa maisha ya sasa huwezi uita mshahara.

Hao wote uliowataja wanatakiwa walipwe mishahara na sio hayo malipo kama posho.
Upo sahihi bwashee ,bora auze mchicha kuliko kutumikishwa kwa kusubiri 200k kwa mwezi
 
Mkuu Mimi nafanya kazi za ndani nalipwa laki je niache kazi au Mimi nifanyeje jamani?

MTU anayefanya kazi za ndani akalipwa 100k
Amemzidi kwa mbali Sana anayelipwa 200k

Mfanyakazi wa ndani anayelipwa 100k
✓ Take home 100k.
✓ Chakula anakula Milo yote hapohapo.
Kwa Siku mtu akila kawaida ni 4000 hapo kajibana. Kwa mwezi 120k

✓ Accommodation
Chumba cha Mfanyakazi halipi. Chumba cha kawaida 50k. Kwa mwezi.

✓ umeme halipi kwa mwezi kawaida 10k

✓. Nauli hatoi anakaa hapohapo.
Kwa Siku nauli 1k nauli ya kawaida. Kwa mwezi 30k

✓ maji halipi. Angepanga wastani maji 5k

Na mengineyo.

Jumla ya vitu ambavyo boss anatoa kwa mwajiriwa 350k.
 
Heh au na mimi nikaombe hii kazi imenivutia namna umedadavua
 
Jamaa una akili sana ni vile tu umetokea kihurio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…