Mshahara ungetolewa kila wiki. Kutolewa kila baada ya mwezi kunadumaza uchumi

Mshahara ungetolewa kila wiki. Kutolewa kila baada ya mwezi kunadumaza uchumi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kama umewahi kufanya biashara utakubaliana nami kuwa biashara inachanganya sana tarehe za mwisho wa mwezi.

Baada ya hapo zinadumaa kwa mwezi mzima. Biashara zote, kuanzia za umachinga, za bucha hadi za vifaa vya ujenzi huchanganya mwisho wa mwezi kisha zinadumaa kwa karibu mwezi mzima.

Hii haina afya kwa uchumi sababu uchumi unategemea pesa zizunguke muda wote. Kinachotokea ni kuwa kila baada ya mwisho wa mwezi tunaingia kwenye recession fulani hivi.

Ni kweli kiasi utakachopokea ndani ya mwezi ni kilekile, lakini impact yake kwenye uchumi iwapo kitatolewa kila wiki na kikitolewa kila mwezi ni tofauti sana.

Zamani mishahara ilitolewa dirishani hivyo kulikuwa na sababu za msingi kuitoa kila mwezi. Dunia ya sasa ya kidigitali hakuna sababu itolewe kila mwezi. Mishahara itolewe kila wiki.
 
Huko mbali ilitakiwa tulipwe kwa masaa au kwa task ulizofanya kama nchi zilizoendelea wanavofanya. Kusubiri mpaka wiki au mwezi ni utumwa!
 
Back
Top Bottom