Mshahara wa laki Tano au kujiajiri bodaboda

Mshahara wa laki Tano au kujiajiri bodaboda

Paul dybala

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2023
Posts
524
Reaction score
2,097
Wakuu ...poleni na majukumu ya hapa na pale

Niende moja kwa moja kwenye mada..Mimi Kuna kipindi niliajiriwa Sasa mwaka Jana mwezi wa sita Mimi na jamaa zangu tukatimuliwa...nikalipwa kifuta jasho changu na ndipo nikanunua boda.

Sasa swala linakuja ni moja ...Mimi nikikaa,, kijichanganya kijiweni nikiamka mapema mpka usiku sikosi efu 30000 na kula na mafuta tayri...

Ila Kuna kazi nimepata ni ya Kila siku asubuhi Hadi usiku mshahara laki Tano.??je hapo wakuu nikimbilie wapi?
 
Wakuu ...poleni na majukumu ya hapa na pale

Niende moja kwa moja kwenye mada..Mimi Kuna kipindi niliajiriwa Sasa mwaka Jana mwezi wa sita Mimi na jamaa zangu tukatimuliwa...nikalipwa kifuta jasho changu na ndipo nikanunua boda..
Sasa swala linakuja ni moja ...Mimi nikikaa,, kijichanganya kijiweni nikiamka mapema mpka usiku sikosi efu 30000 na kula na mafuta tayri...

Ila Kuna kazi nimepata ni ya Kila siku asubuhi Hadi usiku mshahara laki Tano.??je hapo wakuu nikimbilie wapi?
 
Okay.

Kuamua huyo mshahara kuna matatu tu:
Moja:Je bado unataka kufanya carrier yako ya huo mshahara wa 500k, kwamba ukienda unaona utatengeneza CV ya wewe kukua na badae upande zaidi, hata kama sio kwenye nafasi za kampuni hiyo au nyingine?
Kama hilo bado lipo kichwani mwako na carrier yako unaijali, chagua hiyo mishe.

Mbili:Ikiwa kwenye hiyo 30000 kwa siku, je kwa mwezi umeshawahi kuona laki 9, au una zaidi ya laki tano mkononi, kama haujawahi, kafanye hiyo kazi...vinginevyo piga boda kaka.

Tatu:Akili yako, imefunguka vipi kutambua kwamba kuajiriwa ni matrix, ya unyonyaji? Kama bado, tafuta ukweli huu, itakurahishia kwenye kuona moja na mbili ipi ni sahihi zaidii.

Good day
 
Asante mkuu
 
Mkuu piga boda kwa malengo upate kitengo chako utulie boda uumpe mtu akuingizie hata elf10 kwa siku kazi za kuajiriwa zitakufanya u-relax sana na ushindwe kujiongeza

Binafsi nmeacha kuhangaika na taaluma yangu nakomaa na biashara nikishuka napambana na nikipanda napambana zaidi kwenye ajira nimeamua kukueka pending ntaajiriwa nikiweka vitega uchumi vitakavyo ingiza mtonyo bila mm kushiriki moja kwa moja.
 
Pambana na boda wewe nunua zingine wape watu wakuletee chochote kitu iwe kama saving yako kweli kifo nje nje ila umakini tu
 
Pengine Mungu anawatumia watu kukuepusha na kuingia chini ya fuso la kokoto wewe unaanza kupima mshahara.

Mungu ameshakuona ukiingia chini ya fuso la kokoto siku za karibuni kama utaendelea na hiyo bodaboda, usipuuze! Kila fursa ina sababu yake.
 
Back
Top Bottom