Mshahara wa laki tatu Dar

Mshahara wa laki tatu Dar

Wakubwa mtu akipaata deal la laki 3 Dar es salaam, ni kama mpya hajawahi fika na hana sehemu yeyote ya kufikia. Kwa mshahara wa laki 3 anaweza toboa Dar??
Daslam nenda na nguvu na akili zako mengine yote utayakuta huko daslam ndo mji pekee unaweza enda Bila hela na ukarudi tajiri

Lakini pili daslam unaweza enda tajiri ukarudi maskini

Maamuzi ni yako
 
Kuhusu kutoboa kwa mshahara wa laki tatu uongo labda tu mwambie ataweza kuishi japo kwa masimango

UKianza kufanya malipo ya vitu kama pango,umeme,chakula,maji,bajeti ya usafiri n.k atajikuta mwisho wa mwezi anadaiwa kiasi sawa na mshahara wake wa awali.
 
Hilo swali hautopata majibu sahihi Ila kila MTU Ana life path yake .

Hiyo Kazi ni stepping stones itumie kukufikisha sehemu Fulani .

Ukifika DSM jenga network na watu wenye potential , kuwa nidhamu ya pesa , kaa mbali na mambo yote negative Kama , kamali, pombe ,uzinzi n.k.

Blueprint
 
Unatoboa vizuri kabisa!
Kuna watu wanaamka hawajui cha kufanya na maisha yanaenda.
Kikubwa afya na mpangilio sahihi wa kipato chako na kukubali status yako kwa wakati husika.
DSM ni mji ambao kwa yeyote mtu anavyotaka kuishi anaishi kuanzia malazi,mavazi na chakula.
Ni wewe tu na kipato chako kitakupa mwongozo sahihi wa namna ya kuishi.
 
Hilo swali hautopata majibu sahihi Ila kila MTU Ana life path yake .

Hiyo Kazi ni stepping stones itumie kukufikisha sehemu Fulani .

Ukifika DSM jenga network na watu wenye potential , kuwa nidhamu ya pesa , kaa mbali na mambo yote negative Kama , kamali, pombe ,uzinzi n.k.

Blueprint
Afanye kazindani ya miezi 8 afungue hata genge kubwa kama side hustling mana sisi wengine tuko dar mda mrefu na hao watu potential hatujawapata. Dunia ina watu wabinafsi sana.... jamaa apambane yeye kama yeye
 
Yes-sema nyie watu wa Biashara mna nafasi kubwa ya kukutana watu Potential .
Mtu akiona muhitaji wa kitu flani kile kitu hakupi. Anajua akikunyima wewe itakuathiri kimawazo, kifedha, kinamna namna so anakumyima ili iwe beyond your expectation ujutie maisha yako yote kumjua. So, kwenye hatua ya kwanza ya maisha ya sasa ni kukubali kwamba si kila mtu ana roho safi. Mm nishakutana mpaka na mtanzania namba 3 mpaka leo niko kariakoo
 
Back
Top Bottom