Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Mshahara wa mfanyakazi na wengine wenye kipato fixed kama wapokea pension huwa unapungua kila mwaka. Kinachokula mshahara wa watu hawa ni mfumuko wa bei. Kwenye mfumuko wa bei thamani ya pesa huwa inapungua.
Mfumuko wa bei wa 5% maana yake pesa imepungua nguvu kwa asilimia tano. Kama unapata mshahara wa 1m na mfumuko wa 5% ukatokea, basi hauna tofauti na mtu aliyepunguziwa mshahara kutoka 1m kuja 950,000 katika mazingira yasiyo na mfumuko.
Kama hujaongezewa mshahara kwa miaka mitano, na mfumuko wa miaka mitano ni 20%. Basi jua mshahara umeshushwa hadi 800,000.
Wanaopokea pensheni za kila mwezi ndiyo hatari zaidi sababu hakuna matumaini ya kuongezewa pensheni. Mfumuko unaweza kula pensheni na kukuacha masikini kila mwaka.
Hata ukiongezewa mshahara 3% na mfumuko ukawa 5%, jua kuwa mshahara umepungua kwa 2%.
Zamani wafanyakazi ndiyo walikuwa wenye maisha mazuri sana, siku hizi mfanyakazi hamkuti Chinga mwenye goli zuri kwa mapato. Chinga mapato yake yanaenda sambamba na inflation zinavyoenda. Mfanyakazi mshahara wake upo palepale au unaongezeka kidogo huku inflation inakimbia.
Serikali na waajiri wengine wanawezaje kulinda watumishi na wastaafu kutokana na inflation?