A
Anonymous
Guest
Posho ya madaraka kwa waganga wafawidhi.
Kwa muda mrefu sasa, waganga wafawidhi wa zahanati na vituo vya afya nchini wamekuwa wakitekeleza majukumu mengi mazito ya kiuongozi bila kutambuliwa ipasavyo kwa malipo yao. Mbali na kuhudumia wagonjwa, sisi ndio tunasimamia watumishi, tunaratibu mipango kazi ya mwaka, tunasimamia ujenzi na miradi ya vituo, tunashughulikia mifumo ya hospitali, pharmacy, na kazi zote za clerking, pamoja na safari mbalimbali zinazohusiana na utendaji wa kituo.
Licha ya majukumu haya yote, mshahara wetu hauna tofauti na mganga wa kawaida ambaye jukumu lake kuu ni kuhudumia wagonjwa pekee. Hii ni hali isiyo ya haki na inaathiri morali ya wafanyakazi wa afya, hasa katika ngazi ya msingi ambako huduma za afya zinaanzia.
Tunaiomba Serikali na mamlaka husika zitambue mchango wetu na kutupatia stahiki yetu ya posho ya madaraka kama ambavyo inavyotolewa kwa viongozi wa sekta nyingine za umma.
Ni wakati wa kuwatendea haki wale wanaosimamia huduma za afya kwa bidii na uaminifu kwa manufaa ya wananchi wote.
#HakiKwaWagangaWafawidhi