Mshambuliaji gani ataanza kwenye kikosi chako kati ya hawa?

Suarez jamaa sio wa kusubiri mipira ni msumbufu kwa mabeki na akupa options nyingi katika kumtumia .

Nakumbuka kuna msimu EPL alifungiwa mechi 10 lakini akarudi na kuubuka kidedea kwenye mbio za ufungaji bora.
Huu msimu nilimvulia kofia alirudi na hatrick kama tatu hivi kufidia mechi alizofungiwa 😁 jamaa anajua sema utukutu tu ulikuwa unamsumbua
 
Umemaliza.

Naona wengi hawamkumbuki yule Suarez wa Liverpool..
 
Madridista here ila Suarez analijua goli bhana. Anaweza akaangalia goli lilipo kabla hajapokea pass na akipokea akafunga wakati ameshahama position wakati anafanya makadirio. Jamaa ni pure no 9 anayekupa nafasi hata kumchezesha kutokea pembeni.
Kumbe kuna wakati dish haliyumbi kipindi cha mvua..
 
Luis Suarez .......

Hii ni habari nyingine kabisa...

Machine suares
 
Suarez ktk ubora wake hakuna anaemfkia hapo.
Suarez pale mbele unaweza kumtumia nafasi yoyote pembeni kulia au kushoto, striker wa mwisho hata nyuma ya striker namba 10.

Suarez anafunga magoli ya aina yoyote, ni king'ang'anuzi yaan msumbufu sana pale mbele akisimama.

Pale EPL na laliga wanajua mziki wake, alikua mfungaji bora mbele ya messi na cr7 wakiwa ktk ubora wao ule wa kishndana kufunga.. kiufupi tu tukiachana na ushabiki huyo suatez ni level nyingine kabisa
 
Mimi ni Barca na hao wote nimewatazama sana.

1. Lewandowski
2. Suarez
3. Benzema
4. Ibrahimovic
 
1.Zaltan Ibrahimovic
2.Zaltan Ibrahimovic
3.zaltan Ibrahimovic
4.benzema
5.Suarez
6.Bob



Sababu ni hii mwamba ana energy ana skills anafunga magoli ya Sina yeyote
Umewatazama ktk ubora wao wote? Lewandowski ni mtu mwingine, wa kumzidi hapo labda angekuwepo Kunkun Aguero.
 
Umewatazama ktk ubora wao wote? Lewandowski ni mtu mwingine, wa kumzidi hapo labda angekuwepo Kunkun Aguero.
Kwenye finishing, nakubaliana na wewe. Lewandoski yuko very clinical. Nafasi tano atakazopata, nne anatia kambani. Shida ya Lewandoski, hana vitu vingi vya kuoffer tofauti na kufunga.

He's a typical number nine, anacheza karibu na box. Kura yangu nimeiweka kwa Suarez kwa sababu anaweza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja.

Anaweza kurudi midfield, akachukua mpira na kupanda nao juu kutupia. Anaweza kukipiga akitokea pembeni kushoto na hata kulia kitu ambacho ni adimu kumuona Lewandoski akifanya.

Suarez akishindwa kufunga yeye, basi atawachezesha wengine wakufunge. Ndio maana Danny Sturrige alionekana mtu pale Liverpool wakati anacheza na Suare, na hakuwahi kukifikia kile kiwango tena tangia walipotengana.

Kwa upande wangu, nadhani ni Ronaldo De Lima pekee ndie anaeweza kumfunika Suarez kwa strikers niliopata kuwaona!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…