Nihzrath
Member
- Jan 15, 2013
- 51
- 116
FERNANDO PEYROTEO
MSHAMBULIAJI HATARI KABISA ALIYEPATA KUTOKEA DUNIANI
NA
NIHZRATH NTANI JNR
Kuna matukio ambayo unaweza kuyafanya na ukaendelea kukumbukwa hata baada ya kuondoka Duniani. Matukio hayo yanaweza kuwa mema au mabaya.
Mfano, Aldof Hittler anaendelea kukumbukwa kwa ukatili wake. Hata baada ya kufariki miongo mingi iliyopita.
Kuna watu kama Alexander Bell ( mgunduzi wa mawasiliano ya simu). Akina Isaack Newton na wengine wengi wanaendelea kukumbukwa kwa ugunduzi wao ulioleta faida kubwa ulimwenguni, hata baada ya kuondoka kwao Duniani. Dunia inaendelea kuwakumbuka.
Hata hivyo, pale unapotajiwa jina la Fernando Peyroteo. Hapana shaka hakuna shabiki yoyote wa soka anayeweza kumuelezea. Alikuwa nani mtu huyu? Unaweza kujiuliza. Historia dhidi yake ni kama imefichwa makusudi au kwa bahati mbaya. Hakuna anayejali.
Ni kusini Magharibi mwa nchi ya Angola ndani ya mji wa Humpata . Mnamo Machi 10, 1918. Ni karibu karne moja iliyopita. Ndipo mahala na siku aliyozaliwa mtu huyu aliyepata kuitwa jina la Fernando Bastista Peyroteo.
ALIFANYA NINI MTU HUYU?
Unapojaribu kuwasoma wanasoka maarufu Duniani waliopata kucheza soka enzi hizo. Ni ngumu sana kulipata jina la Fernando Peyroteo. Historia yake haizungumzwi. Mpaka leo hatujui ni kwa sababu ipi? Labda ni bahati mbaya tu. Ama pengine kuna mahala walifanya makosa hata jina lake halizungumzwi?
Unapobahatika kusoma historia yake iliyofichwa unabakia kujawa na msisimko wa kutaka kumfahamu zaidi. Mwisho, baada ya kuisoma historia yake, unabakia kupigwa na butwaa ni kama husiyeamini kinachozungumzwa dhidi yake.
Kumbukumbu zinaeleza. Mwanaume huyu aliyeitwa Fernando Peyroteo alikuwa mshambuliaji hatari kabisa katika historia ya soka Duniani. Mpaka hivi leo hakujawahi tokea mshambuliaji hatari zaidi kuliko yeye.
Takwimu zake na rekodi zake zinazungumza zaidi. Hazijawahi kuvunjwa kwa zaidi ya miaka 90 sasa na nina hakika zitaendelea kudumu vizazi hadi vizazi.
Bahati mbaya mtu huyu aliyekuwa raia wa Ureno jina lake limejaa kwenye vitabu ya historia ya soka la Ureno pekee. Wakati ulipofika mjadala wa nani awe mwanasoka bora wa muda wote wa Ureno ulipofika.
Jina lake liliwekwa kando ya Eusebio Da Silva na Cristiano Ronaldo. Ni hapo ndipo mashabiki wengi wa soka waliopata kusoma habari zake walipopigwa na mshangao? Takwimu zake zinawaacha mbali mno watu hao wawili wanaosemwa ni bora kuliko yeye.
Fernando Peyroteo ndiye mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya Ureno, maarufu kwa jina la Primeira Liga. Akifunga magoli 331 katika mechi 187. Ndio magoli hayo yote katika mechi 187 tu. Hakuna mwanadamu mwingine yoyote aliyewahi kufanya hivyo zaidi yake.
Katika timu ya taifa ya Ureno alicheza mechi 20 na kufunga magoli 15. Ni uwiano bora zaidi kwa mchezaji Duniani. Fikiria kama mtu huyu angelikuwa anacheza soka nyakati hizi angelikuwa na thamani kiasi gani?
NDIYE MFALME WA SOKA KLABUNI SPORTING LISBON.
Ndani ya Estadio De Lumia katika miaka ya 1938 hadi 1949. Ni dimba ambalo kwa sasa linaitwa Jose Alvalade linalomilikiwa na klabu ya Sporting Lisbon. Ni mahala hapo ndipo ambapo Fernando Peyroteo alipofanya mambo ya kushangaza.
Akitumia misimu 12 ya soka lake. Alifunga magoli 635 katika mechi rasmi 393 za mashindano yote. Si Pele, Gerd Muller wala Farenc Puskas walioweza kufanya vile alivyofanya Peyroteo.
Edson Nascrimento 'Pele' anayetajwa mfalme wa soka Duniani alifunga magoli 767 katika mechi 831 zilizokuwa za mashindano rasmi.
Hawa watatu wanatajwa kuwa washambuliaji hatari zaidi katika historia ya soka Duniani, lakini si kitu mbele ya mtu huyu. Takwimu zinatupa majibu baina yao.
Fernando Peyroteo chini ya kocha raia wa Hungary aliyeitwa Jozsef Szabo. Waliunda safu kali kabisa iliyotisha enzi hizo na kubatizwa jina la 'Five Violins' ikiwa na wakali wengine akina Jesus Corriea, Albano Pereira, Manuel Vasques na Jose Travassos.
Pamoja nao waliweza kutwaa mataji mengi zaidi yakiwemo mataji matano ya ligi kuu ya Ureno. Huku yeye akitwaa tuzo ya ufungaji bora mara sita.
ALIKUWA NA REKODI ZA KUSHANGAZA
Alikuwa hatari kweli kweli. Bado rekodi yake ya kufunga goli 9 katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Leca Fc katika ushindi wa goli 14-0 mnamo mwaka 1942. Ingalipo inapumua na ni ngumu kuvunjwa kwa miaka mingi ijayo.
Fernando Peyroteo anarekodi nyingine ya kuifunga Boavista magoli 8 katika mechi moja ya ligi. Pia aliweza kufunga magoli 6 katika mechi tatu tofauti za ligi.
Mtu huyu hakuwa wa mchezo mchezo hata kidogo. Aliwahi funga magoli 5 katika mechi moja mara 12 kwa timu tofauti tofauti huku pia akifanya hivyo kwa hat trick mara 52.
Kwa maisha yake yote ya soka. Unaweza kufikiri haya yanayoelezwa ni simulizi tu za wahenga. Huu ni ukweli halisi. Mtu huyu ameifunga Fc Porto magoli 33 katika mechi 32 alizocheza dhidi ya timu hiyo.
Pia hakuwaacha salama wababe wengine wa ligi hiyo klabu ya Benfica. Hawa aliwafunga magoli 64 katika mechi 55 alizokutana nao. Alikuwa hatari kweli kweli.
NDIYE ALIYEGUNDUA KIPAJI CHA EUSEBIO DA SILVA
Sahau kuhusu Gulla Guttman. Kocha yule aliyewapa laana Benfica anayeelezwa kutoa mchango mkubwa katika kipaji cha Eusebio.
Fernando Peyroteo alistaafu Soka mnamo Octobar 1949 akiwa na miaka 31 tu wakati huo. Mechi yake ya mwisho kucheza alifunga Hat trick.
Mashabiki wengi walilia kwa uchungu. Alipostaafu alirejea Angola hata hivyo miaka michache baadae alirejea tena Ureno na kufundisha timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Ndipo mnamo mwaka 1961 alipomuita kwa mara ya kwanza timu ya Taifa kijana mdogo aliyeitwa Eusebio. Safari ya Eusebio kuwa mmoja ya washambuliaji hatari barani Ulaya ikaanza siku hiyo.
BAHATI MBAYA ALITAMBA KATIKA ZAMA AMBAZO HAKUKUWAPO NA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA
Mwili wake ukiwa umelala katika ardhi ya makaburi ya 'Edlington' ndani ya jiji la Lisbon- Ureno. Kama leo angelifufuka Fernando Peyroteo angelipenda kucheza soka kwa nyakati hizi.
Mtu huyu hakuwahi kucheza mashindano ya kombe la Dunia kwa sababu wakati huo kulikuwa hakuna amani, vita ya Dunia ilitamalaki.
Bahati mbaya hakucheza michuano ya Ulaya kwa kuwa hayakuwapo mashindano hayo. Labda pengine yangelikuwapo na yeye angelishiriki wakati huu tungekuwa tunaimba jina lake kama tunavyoimba jina la Pele, Maradona na wengine wengi.
Nyakati zake hata kwa soka la Ureno kulikuwa hakuna matangazo ya runinga. Matangazo ya runinga yalikuja nchini Ureno mnamo mwaka 1957 akiwa tayari ameshatundika darunga zake.
Fernando Peyroteo alifariki mnamo November 28, 1978 kwa mshtuko wa moyo. Akiwa na miaka 60. Bila shaka anabakia kuwa mshambuliaji hatari zaidi kuwahi kutokea. Lakini jina lake haliimbwi. Ni huzuni ilioje!
.