Tuache kubeza kila kitu. Inawavunja moyo viongozi wetu. Huyu jamaa ni jembe!!!
Muangalie hapa:
Ni mapema mno kutoa hukumu juu ya uwezo wake. Sababu zifuatazo zinambeba:
(1) Anatoka nchi yenye kutoa wachezaji bora duniani na yenye kiwango cha juu na Ligi bora kuliko Tanzania. Kwa hivyo hata kama huko ni wa kawaida lazima huku atakuwa zaidi ya kawaida.
(2) Tumekuwa tukisikia habari zake kabla hajaja huku kupitia kwa mchezaji aliyetokea kucheza Ligi ya huko (kuipa Agban). Bila ya shaka Agban mwenyewe ameshaona Ligi zote mbili na kwa hivyo uoni wake juu ya uwezo wa mchezaji anayempendekeza kucheza Ligi yake unafaa kuzingatiwa.
(3) Wasifu wake umeonesha amekuwa akielekea timu kubwa zaidi kadri anavyohama timu moja kwenda nyengine. Maana yake kiwango chake inaendelea kukua kadri anavyohama timu.
(4) Video hii inadhihirisha kwamba ni straika anayemudu vyema ustraika.
Sababu zifuatazo zinamwangusha:
(1) Kwa jinsi ustraika wa aina inayoonekana kwenye video hii ulivyokuwa adimu duniani, unapata mashaka kwa nini haitwi Timu ya Taifa au kutakiwa kucheza Ulaya
(2) Kabla ya kuja kwa Agban, hakukuwa na anayejua habari zake kama ambavyo, mathalan, Afrika nzima ilikuwa ikmjua Samatta
(3) Hakukuwa na figisu zozote kutoka timu inayopoteza mchezaji muhimu kama tunavyoaminishwa, angalau kumwongezea dau au kudai donge nono kutoka Simba. Angalia Mavugo alivyofanyiwa figisu na timu yake mwaka jana.
(4) Mchezaji mwenye uwezo kama tunaoaminishwa lazima angeibeba timu yake kuwa kwenye angalau nafasi tatu za juu; yake ni ya tano. Labda ungesema ndiye mchezaji pekee bora kwenye timu hiyo; lakini haiwezekani timu dhaifu kudumu na mchezaji mmoja pekee mzuri ndani ya miaka yote hiyo bila ya kunyakuliwa na timu kubwa. Angalia Mwalyanzi, Busungu, Kaseke, n.k. hapa kwetu. Au Vardy na Mehrez wa Leicester baada ya kutwaa EPL
(5) Ukiangalia msimamo wa Ligi yao timu yake haingozi kwenye zilizofunga mabao mengi, na kwa maana hiyo haiyumkini kwamba ana magoli mengi kiasi cha kutisha
(6) Mchezaji bora hupatikana kwenye timu angalau nne za juu. Anapotokea wa chini ya hapo kuonesha kiwango bora, hatadumu na timu hiyo muda mrefu. Na kokote atakokwenda atasajiliwa na timu zilioko msimamo wa juu; angalau nne bora. Angalia Wawa, Mavugo, Ame Ali Zungu, Samatta, n.k.
(7) Mchezaji mzuri wa Ivory Coast kufikia umri wa miaka 31 bila ya kutakiwa Ulaya, kuchezea Timu ya Taifa au angalau kushiriki robo fainali ya mashindano yoyote ya vilabu Afrika maana yake ni kuwa hana kiwango cha kutisha hivyo.
(8) Video hii inatuonesha mchezaji mwenyewe akiwa kwenye kiwango cha juu cha uwezo wake. Imetengenezwa mahsusi kwa kujiuza. Hatuna video inayoonesha kiwango chake cha wastani au cha chini kabisa. Ukisikiliza wimbo wa Muumini wa Tunda akiwa na Tamtam, unaweza kuamini kwamba ni zaidi ya wote wengine. Lakini ....?
Maoni yangu: