mmariii
Member
- Jul 12, 2015
- 71
- 57
Mshambuliaji wa ManCity Sergio Aguero ajeruhiwa katika ajali
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amejeruhiwa katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam, saa chache baada ya kuhudhuria tamasha.
Raia huyo wa Argentina, mwenye umri wa miaka 29, anaarifiwa kuwa ndani ya taxi akielekea katika uwanja wa ndege baada ya kuhudhuria tamasha la muimbaji Maluma.
City imesema "alikuwa Uholanzi katika siku yake ya mapumziko na amepata majeraha".
Polisi Amsterdam wameithibitishia BBC kwamba watu wawili walikuwa ndani ya taxi iliyohusika katika ajali katika eneo la De Boelelaan mjini humo.