...na sasa hivi tumeona mwanga. Tunawaombea uzima viongozi wote wa upinzani waliochaguliwa; ambao CCM imeona haya kuiba kura zao.Tunawaombea heri na baraka katika kazi yao.
Kitu cha kwanza watakapoingia mjengoni ni kudai na kushinikiza uwepo wa TUME huru ya uchaguzi. Kama Zanzibar uliweza kupatikana muafaka, inshallah na hili litafanikiwa Tanzania Bara.
Vyombo vya habari, taasisi huru za kiraia lazima ziandike kuhusu kuwepo kwa tume huru, hadi haki ipatikane. Kwakuwa huu mfumo ni wa vyama vingi, haiwezekani hata kidogo viongozi wa tume na taasisi nzima, kuwajibika kwa serikali.
Na wale wananchi wenzangu na mimi ambao pamoja na ku enjoy machungu ya maisha magumu yanayosababishwa na serikali ya mabavu ya CCM; lakini hawaoni mfano wa wenzao ambao wameamua kusema sasa basi, nawatakia mateso mema. Hongereni Ubungo, Kawe, Kigoma kaskazini, Hai, Rombo, Arusha mjini na kweingineko, mliotutoa kimasomaso watanzania.
Naungana mkono na mchangiaji mmoja hapo juu kwa kuwatafadhalisha wabunge wa CCM, wafanye kazi kwa maslahi ya watanzania. watambue kwamba 2015 si mbali.
Tanzania bila Kikwete na mafisadi wenzake na CCM yao inawezekana.