Mshare wa speedometer kushuka mpaka zero gari linapokimbia speed zaidi ya 120km/hr

Mshare wa speedometer kushuka mpaka zero gari linapokimbia speed zaidi ya 120km/hr

swamila

Senior Member
Joined
Apr 4, 2015
Posts
176
Reaction score
81
Gari yangu aina ya Premio old model inatumia engine 7A nikiwa katika masafa marefu nikifikisha speed zaidi ya 120km/hr mshale wa speed unashuka gafla mpaka zero halafu inawasha Overdrive inanilazimu nipaki pembeni nizime gari halafu niwashe tena ndo inarudi kwenye hali yake. Naomba msaada wapendwa kama kuna mtu humu au mtaalam aliwai kukutana na tatizo kama hilo.
 
Mshale wa speed unashuka mpk zero huku gari ikiendelea kukimbia au unashuka mpk zero na gari inasimama?
 
Vehicle Speed sensor hio mkuu. Ndo ishakutumia ujumbe kama imekwisha habari yake. Tafuta nyengine uweke uendelee na safari
 
Sasa wewe speed zote hizo za nini...? Kwa barabara hizi za uchumi wa kati...unataka kurest in peace...?

Anyway tafuta fundi afanye diagnosis utapata jibu soon ni nini cha kufanya....kama ni speed sensor utapata uhakika kuliko kukisia
 
Back
Top Bottom