Mshenga!!!!!

Mshenga!!!!!

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,023
Reaction score
12,811
Jamani naomba kujua mshenga anatakiwa awe na vigezo gani maana kuna mtu mmoja aliniomba eti niwe mshenga wake nikakataa kwa kujua kuwa mshenga anatakiwa awe ameoa.....
Wale ambao mmewahi kuwa washenga naomba mnipe sifa za mshenga ili muda wa kutafuta mshenga nisipate taabu na ikiwezekana huenda nikapata hapahapa JF!!
 
katavi kila la kheri naona uko kny harakati,,subiri wenye uelewa waje wakupe uzoefu
 
Anatakiwa awe kabila la mwanamke anayejua mila na desturi zao wasije wakampiga changa la macho kwa mila asizojua
 
Naingoja shule toka hapa nami pia,au ungemuuliza dad yako kama ina haraka zaidi maana yeye kapitia huko!
 
we desi hiyo ni lazma kumbe?mi nildhani ni maadili zaidi

Pamoja na maadili lakini ni muhimu kuwa kabila la mwanamke watamwambia alete mbegu za bangi (kwa shemeji zangu wakurya) anabaki kushangaa lazima ajue mila zao bana wewe vipi subiri muda wako ukifika
 
Jamani naomba kujua mshenga anatakiwa awe na vigezo gani maana kuna mtu mmoja aliniomba eti niwe mshenga wake nikakataa kwa kujua kuwa mshenga anatakiwa awe ameoa.....
Wale ambao mmewahi kuwa washenga naomba mnipe sifa za mshenga ili muda wa kutafuta mshenga nisipate taabu na ikiwezekana huenda nikapata hapahapa JF!!

Ushenga ni zoezi kubwa, ujue mila na desturi za kabila la mwanamwali. Mshenga ni mtu muhimu kwenye mawasiliano yote ya posa na suala zima la mahari hatimae ndoa kati ya upande wa familia ya mwanaume na mwanamke wanaotarajia kuoana. Washenga wengi niliowaona ni wanaume pia!!
Kwahiyo Katavi ukikubali suala la ushenga ulikubali na kutekeleza majukumu yake. Unataka kuona nini?
 
Pamoja na maadili lakini ni muhimu kuwa kabila la mwanamke watamwambia alete mbegu za bangi (kwa shemeji zangu wakurya) anabaki kushangaa lazima ajue mila zao bana wewe vipi subiri muda wako ukifika

hahaha,,hivi mf,katavi hawezi kuchukua mshenga wa jinsia yetu ili tujitolee,au haifaagi?
 
Nani kasema?? Hiyo haipo bana nyie watu nyie kwa kupindisha mambo shauri yenu jaribuni muone kama inawezekana
 
Naingoja shule toka hapa nami pia,au ungemuuliza dad yako kama ina haraka zaidi maana yeye kapitia huko!
Haina haraka sana, nataka nifahamu kwanza sifa za mshenga. Hivi baba mzazi anafaa kuwa mshenga?
 
Nani kasema?? Hiyo haipo bana nyie watu nyie kwa kupindisha mambo shauri yenu jaribuni muone kama inawezekana

nimekusikia mydr,ila nimepewa somo kwa ukali dah!nimehs fimbo inaninyemelea,btw mbona hunipi progress???????
 
Ushenga ni zoezi kubwa, ujue mila na desturi za kabila la mwanamwali. Mshenga ni mtu muhimu kwenye mawasiliano yote ya posa na suala zima la mahari hatimae ndoa kati ya upande wa familia ya mwanaume na mwanamke wanaotarajia kuoana. Washenga wengi niliowaona ni wanaume pia!!
Kwahiyo Katavi ukikubali suala la ushenga ulikubali na kutekeleza majukumu yake. Unataka kuona nini?
Nami pia nitahitaji mshenga hapo baadae, hivyo muhimu kujua vigezo!
 
Haina haraka sana, nataka nifahamu kwanza sifa za mshenga. Hivi baba mzazi anafaa kuwa mshenga?

mh!baba tena????katavi!wapi dena umsaidie katavi asije kunyimwa mke jamani
 
Back
Top Bottom