Anatakiwa awe kabila la mwanamke anayejua mila na desturi zao wasije wakampiga changa la macho kwa mila asizojua
we desi hiyo ni lazma kumbe?mi nildhani ni maadili zaidi
Jamani naomba kujua mshenga anatakiwa awe na vigezo gani maana kuna mtu mmoja aliniomba eti niwe mshenga wake nikakataa kwa kujua kuwa mshenga anatakiwa awe ameoa.....
Wale ambao mmewahi kuwa washenga naomba mnipe sifa za mshenga ili muda wa kutafuta mshenga nisipate taabu na ikiwezekana huenda nikapata hapahapa JF!!
Jinsia yoyote anafaa???
Pamoja na maadili lakini ni muhimu kuwa kabila la mwanamke watamwambia alete mbegu za bangi (kwa shemeji zangu wakurya) anabaki kushangaa lazima ajue mila zao bana wewe vipi subiri muda wako ukifika
hahaha,,hivi mf,katavi hawezi kuchukua mshenga wa jinsia yetu ili tujitolee,au haifaagi?
Nani kasema?? Hiyo haipo bana nyie watu nyie kwa kupindisha mambo shauri yenu jaribuni muone kama inawezekana
Nami pia nitahitaji mshenga hapo baadae, hivyo muhimu kujua vigezo!Ushenga ni zoezi kubwa, ujue mila na desturi za kabila la mwanamwali. Mshenga ni mtu muhimu kwenye mawasiliano yote ya posa na suala zima la mahari hatimae ndoa kati ya upande wa familia ya mwanaume na mwanamke wanaotarajia kuoana. Washenga wengi niliowaona ni wanaume pia!!
Kwahiyo Katavi ukikubali suala la ushenga ulikubali na kutekeleza majukumu yake. Unataka kuona nini?
Haina haraka sana, nataka nifahamu kwanza sifa za mshenga. Hivi baba mzazi anafaa kuwa mshenga?