Mshindi wa Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (JF Stories of Change) kujulikana Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Yule mshindi wa Shindano la “JF Stories Of Change” atakayejinyakulia kitita cha Tsh. Milioni 5 anatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa Oktoba 15, 2021 katika hafla fupi itakayoanza saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku.

Hafla hiyo ya kutangaza na kukabidhi washindi zawadi itaambatana na Chakula cha Jioni, Vinywaji na Burudani.


Kuhusu Shindano

Jamii Forums (JF) ilitoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko (Stories of Change).

Shindano lilikusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye

Pia, shindano lililenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Shindano hili lilianza Julai 14 hadi Septemba 30


Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-


Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 5

Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 3

Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop na Simu za mkononi

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal)

Zaidi, soma; Mrejesho: Je, ulishiriki shindano la “JF Stories of Change?” Kaa karibu na PM yako
 
Upvote 41
Kila la kheri kwa washiriki wote, hongera kwa watakaoibuka kidedea. Niwapongeze wote waliweza kuandika hata kama kura hazikutosha, wasikate tamaa.

Pongezi kwa team yote ya JF, ni mwanzo mzuri.

Kama kuna mapungufu yamejitokeza, naamini yataboreshwa kwenye mashindano yajayo.
 
Kila la heri kwa washiriki wote. Na hongera kwetu wote ambao tuliandika stories/mada zetu.

Hata kama hautashinda (hatuwezi kushinda wote) lakini tumepata kujifunza mambo mengi sana yenye kuleta mabadiliko chanya kwetu binafsi na katika jamii kwa ujumla wake.

Nirudie kusema hongera kwetu sote kwa kushiriki.
 
Mkuu ulishiriki na wewe?
 
Muweke vigezo mlivyovitumia kupatikana kwa washindi na namna mchakato mzima unavyokwenda. Ili shindano linalokuja mwandishi ajue namna zoezi linavyoendeshwa.

Swala la ushindani wa uandishi lisifanyike kama michezo ya kubashiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…