Mshindi wa tuzo ya amani Denis Mukwege atishiwa kuuawa, Umoja wa Mataifa wamuhakikishia usalama

Mshindi wa tuzo ya amani Denis Mukwege atishiwa kuuawa, Umoja wa Mataifa wamuhakikishia usalama

Rahma Salum

Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
30
Reaction score
59
Umoja wa Mataifa umeagiza kikosi maalumu kwa ajili ya kuhakikisha usalama kwa mshindi wa tuzo ya amani Denis Mukwege baada ya kupokea vitisho kutokana hatua alizochukua kudai haki kwa uhalifu unao tendeka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jitihada za kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita na machafuko ya kijeshi zilimpa Denis Mukwege heshima na kutunukiwa tuzo ya Amani (Noble Peace Prize) 2018.

Amepokea vitisho vya kuuawa yeye na familia yake kupitia simu pamoja na mitandao ya kijamii, kutokana na hatua alizochukua kupinga kitendo cha mauaji yaliyotokea Mashariki mwa Kongo na kutoa wito kwa serikali kulinda haki za binadamu. Umesema Umoja wa Mataifa.

Mukwege amepokea vitisho kama hivi miaka ya nyuma. Mwaka 2012 alinusurika kuuawa baada ya watu wenye silaha kuvamia nyumbani kwake na kurusha risasi kupelekea kifo cha mlinzi wake.

Tarehe 9 mwezi Septemba Mukwege ametoa chapisho kupitia mtandao wa Twitter lenye ujumbe wa kushukuru Umoja wa Mataifa kumpelekea kikosi kwa ajili ya ulinzi wake na familia yake.

Chanzo: CNN
 
Back
Top Bottom