Mshirika Mkuu wa Usimamizi wa Maudhui ya META Afrika kufunga huduma zake

Mshirika Mkuu wa Usimamizi wa Maudhui ya META Afrika kufunga huduma zake

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Meta-e1657103014362.jpg


Mkandarasi mkuu wa Meta wa usimamizi wa maudhui Afrika, Sama, alitangaza mapema Jumanne kufungwa kwa kitengo chake cha usimamizi wa maudhui katika kitovu chake nchini Kenya, akitaja hitaji la kurahisisha shughuli.

Haya yanajiri miezi kadhaa baada ya Sama na Meta kufunguliwa mashitaka katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa kuzuia chama cha wafanyakazi pamoja na unyonyaji, na wiki chache baada ya kesi nyingine kutaka Meta kuongeza uwezo wake wa kusimamia maudhui nchini Kenya.

Kufuatia tangazo la Sama, wafanyakazi 200, wanaowakilisha asilimia 3 ya timu yake watakuwa wamepoteza ajira kutoka katika kampuni hiyo.

Uamuzi wa kusitisha mkataba wa Meta ambao unamalizika mwishoni mwa mwezi Machi, unakuja miezi kadhaa baada ya kesi iliyowasilishwa na Daniel Motaung, raia wa Afrika Kusini na aliyekuwa msimamizi wa maudhui ya Sama nchini Kenya mwaka jana akishutumu makampuni hayo mawili kwa kulazimisha watu kufanya kazi, biashara haramu ya binadamu, mahusiano yasiyo ya haki ya kazi, kuzuia chama cha wafanyakazi na kushindwa kutoa "kwa kutosha" msaada wa afya ya akili na wa kisaikolojia.

Uamuzi huo wa Sama pia umekuja wakati ambapo Meta inakabiliwa na kesi nyingine nchini Kenya kwa madai kuwa kampuni hiyo kubwa ya mitandao ya kijamii imeshindwa kutumia mbinu za kutosha za kiusalama kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook jambo ambalo limechochea migogoro iliyosababisha vifo vikiwemo vya Waethiopia 500,000. wakati wa Vita vya Tigray vilivyomalizika hivi karibuni.

Kesi inadai tovuti ya kijamii ilikuza maudhui ya chuki na imeshindwa kuajiri wafanyakazi wa kutosha wenye uelewa wa lugha za ndani ili kusimamia maudhui.

=========

Meta's main content moderation partner in Africa shuts down operations

Meta's main subcontractor for content moderation in Africa, Sama, shuts down content review services

Meta’s main subcontractor for content moderation in Africa, Sama, announced earlier Tuesday the closure of its content moderation arm at its hub in Kenya, citing the need to streamline operations.

This comes months after Sama and Meta were sued in the East African country for union busting and exploitation, and just weeks after another lawsuit called for Meta to increase its content moderation capacity in Kenya.

Following the announcement by Sama, 200 employees, representing 3% of its team, will be let go as the company exits content review services and concentrates on labeling work (computer vision data annotation).

The company sourced moderators from across Africa, and the closure of the arm is said to leave a section without work permits. Sama’s moderators were required to sift through social media posts on all its platforms, including Facebook, to remove those perpetrating and perpetuating hate, misinformation and violence.

Reports indicate Sama encouraged staff affected by the closure to apply for other job opportunities at its Kenya and Uganda offices.

“The current economic climate requires more efficient and streamlined business operations,” said Sama, according to a report by the Financial Times, which said that the social media giant has contracted Luxembourg-based Majorel to fill up the gap.

The decision to drop Meta’s contract, which expires at the end of March, comes months after a lawsuit was filed by Daniel Motaung, a South African national and ex-Sama content moderator, in Kenya last year accusing the two firms of forced labor and human trafficking, unfair labor relations, union busting and failure to provide “adequate” mental health and psychosocial support.

Sama’s decision also comes at a time when Meta is facing another lawsuit in Kenya over claims that the social media giant has failed to employ enough safety measures on Facebook, which has, in turn, fueled conflicts that have led to deaths, including of 500,000 Ethiopians during the recently ended Tigray War.

The lawsuit claims the social site amplified hateful content and failed to hire enough personnel with an understanding of local languages to moderate content.


TechCrunch
 
Back
Top Bottom