Mshirika wa Al-Shabaab afunguliwa mashitaka New York

Mshirika wa Al-Shabaab afunguliwa mashitaka New York

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mshirika wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab anayeshutumiwa kula njama kufanya shambulizi la mtindo wa Septemba 11 nchini Marekani amepelekwa New York kukabiliwa na mashtaka ya ugaidi, wizara ya Sheria ilitangaza Jumatano.

Raia huyo wa Kenya Cholo Abdi Abdullah alihamishwa Jumanne kutoka Ufilipino ambako alikuwa chini ya ulinzi wa askari wa huko tangu alipokamatwa Julai 2019. Ufilipino ilimkabidhi kwa maafisa wa Marekani Jumanne.

Abdullah anatuhumiwa kwa kula njama za kutaka kuteka nyara ndege ya abiria na kuiangusha kwenye jengo moja nchini Marekani . Ikiwa ni sehemu ya njama iliyoongozwa na viongozi wakuu wa al-Shabaab, Abdullah anadaiwa kupata mafunzo ya urubani huko Ufilipino.

Alishtakiwa katika mashitaka sita yaliyofunguliwa Jumatano na alitarajiwa kufikishwa kwa jaji wa serikali kuu huko New York.

Mashtaka dhidi yake ni pamoja na kutoa msaada wa vifaa kwa taasisi ya ya kigaidi ya kigeni na kula njama za kuua raia wa Marekani na njama za kuteka nyara na kuharibu ndege.
 
Hawa jamaa wa Kenya si waaliandama sana Tz kisa yule dogo Mberesero wa Garissa!? Kumbe wao wanapiga game ya Intentional zaidi!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom